Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeeleendea tena hii leo kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja vinne tofauti.
Kule
katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya mabingwa watetezi wa
taji Simba walikuwa wakikumbana na maafande wa jeshi la magereza
Tanzania Prisons mchezo ambao umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi
wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Amri Kiemba.
Matokeo
ya mchezo huo yanaifanya Simba ifikishe jumla ya alama 31 hivyo kuibua
matumaini ya kuendelea kulitetea taji lake, kufuatia kupata sare
mfululizo kabla ya mchezo wa leo.
Katika
uwanja wa Azam Complex kule Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam
wenyeji Azam fc ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya
kombe la shirikisho walikuwa wenyeji wa JKT Ruvu ambapo wamefanikiwa
kuichapa kwa mabao 4-0.
Mabao ya Azam yamefungwa na Hamisi Mcha, John Bocco na Abdi Kassim.
Azam kwa mara nyingine ineendelea kuikaba koo Yanga katika usukani wa msimamo wa ligi wakiwa wote wana alama sawa 36.
Matokeo
ya kushangaza ni katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza ambapo wenyeji
Toto Afrikas walikuwa wakicheza dhidi ya Afrika lyon ya jijini Dar es
Salaam ambapo Lyon imefanikiwa kupata ushindi wake wa tatu tangu kuanza
kwa ligi kuu msimu huu baada ya kuifunga Toto nyumbani kwa mabao 2-0.
Katika
uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wenyeji Coast Union ya huko ilikuwa
dimbani dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha ambapo dakika 90 za mchezo
zimeshuhudia Coast wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 mabao hayo
yakifungwa Selemani Kassim Selembe na Jerry Santo.
Kwa matokeo hayo ni kwamba Coast sasa imefikisha jumla ya alama 30 ikiwa nyuma alama moja kwa Simba.
No comments:
Post a Comment