Klabu ya Simba imekiri kudaiwa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo,
Mserbia Milovan Cirkovic, na kusema kwamba itamlipa kocha huyo kwa awamu
kiasi cha fedha ambacho anawadai baada ya kuvunja mkataba wake.
Hata hivyo, klabu hiyo imesema kwamba Milovan anawadai kiasi cha Dola za Marekani 24,000 na si Dola za Marekani 32,000 kama Mserbia huyo alivyoeleza.

Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala,
amesema kuwa ni kweli wanadaiwa na kocha huyo na kwamba klabu
itahakikisha inamlipa haki yake hiyo kwa sababu alikuwa na mkataba na
klabu hiyo.
Mtawala amesema kuwa wanafahamu ujio wa kocha huyo nchini na kuongeza kwamba bado hawajawasiliana naye rasmi kuhusiana na fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wake.
"Ni kweli anatudai lakini bado hatujakutana naye rasmi mpaka muda huu (jana mchana), ila tutampa haki zake, kuna taratibu zinakamilishwa," alisema Mtawala kwa kifupi.
Mserbia huyo juzi alifika kwenye Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi kati ya timu ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Cameroon ambapo mashabiki wa Simba walipomuona walianza kumshangilia kwa kumpigia makofi.
Simba iliamua kuachana na kocha huyo baada ya kupata matokeo mabaya kwenye mechi za mwisho za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kuingia mkataba na kocha mwingine kutoka Ufaransa, Patrick Liewig.
Mbali na kuipa ubingwa wa Bara, Milovan naye ameweka rekodi ya kukiongoza kikosi kilichoifunga Yanga idadi kubwa ya magoli ambapo Mei 6 mwaka jana waliwapa watani zao kichapo cha magoli 5-0 katika mechi ya mwisho ya ligi pia kuiongoza kutwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Azam 3-2.
Simba imesema kuwa hivi karibuni inatarajia kupokea kiasi cha Dola za Marekani 150,000 ikiwa ni sehemu ya kwanza ya mauzo ya mshambuliaji wake raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, aliyeuzwa katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

No comments:
Post a Comment