Baada
ya kukwama mara mbili, wanachama wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu
(TAFCA) wamepewa fursa ya kufanya uchaguzi wa chama hicho Machi 16
mwaka huu mjini Dodoma.
Kwa
mujibu wa tangazo la uchaguzi huo, fomu kwa ajili ya waombaji uongozi
katika TAFCA zitaaza kutolewa kesho (Febaruari 7 mwaka huu) na mwisho wa
kurudisha ni Februari 11 mwaka huu. Majina ya waombaji uongozi
watakaokuwa wamepitishwa yatatangazwa Februari 12 mwaka huu.
Kipindi
cha kuweka pingamizi ni kuanzia Februari 13 hadi 17 mwaka huu. Usaili
kwa waombaji utafanyika Februari 19 mwaka huu wakati matokeo ya usaili
yatatangazwa Februari 20 mwaka huu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF itasikiliza rufani kama zitakuwepo kati ya Februari
20 na 22 mwaka huu, na uamuzi wa rufani hizo utatangazwa kati ya
Februari 23 na 27 mwaka huu.
Ada
za fomu kwa waombaji uongozi zitakuwa sh. 200,000 kwa nafasi zote
isipokuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na wajumbe wa Kamati ya
Utendaji. Nafasi zitakazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu
Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini, Mhazini Msaidizi, Mjumbe wa Mkutano
Mkuu TFF na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
Fomu kwa waombaji uongozi zinapatikana kwenye ofisi za TAFCA zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment