Wachezaji
wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara na Zanzibar wenye umri kati ya miaka 18 na 21
wametakiwa kuchangamkia fursa ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa
Barani Ulaya, Asia na Afrika wakiwa nyumbani Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Mwandi, Teonas
Aswile, waandaaji wa Michuano ya African Youth Football Tournament amesema kuwa
katika michuano hiyo wachezaji 11 bora watatafutiwa timu moja kwa moja katika
mataifa nane barani Ulaya (Ufaransa, Ureno, Uholanzi, Denmark, Norway, Sweden,
Ubelgiji na Switzerland), Asia na Afrika.
Bwana
Teonas Aswile amesema kuwa wachezaji wa Tanzania bado hawajaonesha muamko
mkubwa licha ya kiwango cha chini cha kushiriki ambacho wamewekewa
ikilinganishwa na wachezaji wa kigeni, ambao licha ya kuwekewa USD 500 bado
wamezidi kumiminika.
“Mpaka
sasa kuna mawakala wawili ambao tumezungumza nao na wamethibitisha kuleta wachezaji
wao zaidi ya 20 kushiriki kwenye michuano.”
“Hii
ni mbali ya wachezaji mmoja mmoja ambao tunaowasiliana nao ambao wanataka kuja,
wakiwa zaidi ya watano. Kwahiyo wachezaji wetu waamke na kuitumia fursa hii
ambayo haipo katika nchi nyingine ya Afrika kwa wachezaji kufanya majaribio
nchini mwao.”
Aidha
Aswile ameviomba vilabu mbalimbali ambavyo vinaweza kuwalipia wachezaji wake
ada ya shilingi laki tatu (Tsh 300, 000) ambayo inahitajika kwa mchezaji ili
aweze kushiriki kwenye michuano ya African Youth Football Tournament kufanya
hivyo kwani mchezaji huyo atakapouzwa klabu husika ndiyo itakayokubaliana na klabu
itakayomchukua na si Kampuni ya Tanzania Mwandi.
“Sisi
tunachokifanya ni kumuwezesha mchezaji aone njia za kufikia malengo yake. Kwa
hiyo akishafanikiwa na amepata timu ya kuchezea iwe Ulaya, Asia au Afrika,
klabu yake ndio itakayokubaliana na timu ya huko sisi hatutachukua chochote”,
Teonas alisema.
Mkurugenzi
huyo akitaja idadi ya wachezaji wa Tanzania ambao tayari wamethibitisha
kushiriki amesema kuwa ni wachezaji watatu jambo ambalo bado linaonyesha mwamko
umekuwa mdogo.
Michuano
ya African Youth Football Tournament itafanyika Tanzania katika uwanja wa
Karume jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 10 hadi 14 mwezi wa sita mwaka huu
na kuwashirikisha wachezaji wenye umri wa miaka 18 hadi 21 ambapo watafundishwa
na makocha watatu kutoka nje ya nchi na wawili wa Tanzania.
Pia
michuano hiyo itashirikisha mawakala kutoka nchi nane za barani Ulaya, Asia na
Afrika ambao wanahitaji wachezaji kwaajili ya klabu wanazoziwakilisha kati yao
wakiwa ni Budak Johan, Cabrera Oliver, Dag Larsson, Phillip Mwakikosa na Dahlin
Martin huku wakala wa kimataifa wa Tanzania Dr Damas Ndumbaro akiwa miongoni
mwa mawakala wa Tanzania watakaoshiriki katika michuano kusaka vipaji kwaajili
ya klabu mbalimbali.
“Tuna
maombi ya mawakala wawili ambao wanataka wachezaji mabeki, washambuliaji na
viungo kwaajili ya klabu zao Kuwait, Qatar, Libya na sehemu nyingine kwa hiyo
hii ndio fursa ya wachezaji wetu kwenda kucheza soka la kulipwa na lenye
maslahi zaidi kwao.”
Imetolewa
na Idara ya Habari
Kampuni
ya Tanzania Mwandi,
TANCOT
House, Ground Floor,
S.
L. P 79944,
Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment