Rufaa iliyowasilishwa katika mahakama ya kimataifa ya
michezo CAS na mchezaji wa Guinea Ismael Bangoura, kupinga adhabu
aliyopewa ya kutocheza mechi yoyote kwa muda wa miezi minne imefuliwa
mbali.
Mzozo huo ulikuwa unahusiana na sakata ya uhamishwa ya mchezaji huyo.
Mahakma
hiyo pia, pia imeipiga marufuku klabu ya Nantes, iliyopandishwa daraja
dhidi ya kusajili mchezaji yeyote katika awamu mbili zijazo za
kuwasijili wachezaji wapya.
Klabu hiyo ya Nantes na Bangoura, vile vile
wameshurutishwa kulipa dola milioni nane nukta nane tatu kwa klabu ya Al
Nasr inayoshiriki ligi kuu ya Milki za kiarabu.
Mahakama hiyo ya CAS, iliagiza kuwa hukumu
iliyotolewa na shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, kuwa Bangoura
ana hatia ya kuvunja mkataba wakati alipokihama klabu ya Al Nasr na
kujiunga na Nantes mwaka wa 2012 idumishwe.
Hata hivyo mahakama hiyo ilifutilia mbali ombi la Al Nasr la kutaka fidia hiyo kuongezwa zaidi.
Bangoura, ambaye aliwahi kuichezea Dynamo Kiev
na Stade Rennes, alijiunga na Al Nasr, kwa mkataba wa miaka minne
Septemba mwaka wa 2010.
Mwanzo wa mwaka wa 2012, aliwakilisha taifa lake
katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika, baada
ya kupata idhini ya klabu yake, lakini alipoteza nafasi yake baada ya
Al Nasr kumsajili mchezaji mwingine kuchukua mahala pake.
Bangoura kisha akajiunga na Nantes, ambayo
ilikuwa ikishiriki ligi daraja ya pile na alisajiliwa na klabu ya Umm
Salal YA Qatar, kwa mkopo Septemba mwaka huo.
BBCSWAHILI CREDIT
No comments:
Post a Comment