Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa
tangazo la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika
Oktoba 20 mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi
ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka
huu.
Akitangaza
mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi
zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13
wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.
Fomu
kwa wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 16 mwaka huu kuanzia saa 3
asubuhi hadi saa 10 kamili jioni kwenye ofizi za TFF. Mwisho wa kuchukua
na kurudisha fomu ni Agosti 20 mwaka huu. Fomu kwa nafasi ya Rais ni
sh. 500,000, Makamu wa Rais ni sh. 300,000 wakati wajumbe ni sh.
200,000.
Mbwezeleni
amesema kwa wale ambao walilipia fomu katika mchakato uliofutwa na
wanakusudia kugombea nafasi zilezile walizolipia, hawatalipia tena ada
ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa
kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.
Kwa
upande wa uchaguzi wa TPL Board, fomu zitaanza kutolewa Agosti 16 hadi
20 mwaka huu, na nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
ambapo ada ni sh. 200,000 wakati wajumbe wa Bodi ada ni sh. 100,000.
No comments:
Post a Comment