Nililia machozi kwa kuchukuliwa Mbuyu Twite, Ilikuwa rafu moja mbaya sana-Rage
Hivi karibuni nilikutana na kiongozi wa timu ya Simba na Mbunge wa
Tabora mjini, Mhe Ismail Aden Rage, jijini London, haya ni maswali
niliyomuuliza, naye kuyatolea majibu katika sauti:(nasikitika kwa ubora
hafifu wa sauti):
1. Bwana Rage una historia ndefu na klabu ya Simba tangu mchezaji
mpaka kiongozi wa nafasi tofauti. Hebu tueleze kwa ufupi historia yako
ndani ya klabu hiyo.
2. Katika kuweko kwako kote ndani ya Simba ni wakati gani ulishiriki
kuipa klabu hiyo mafanikio makubwa kuliko wakati mwingine ukiwemo ndani
ya klabu hiyo kama mchezaji, Katibu Mkuu au Mwenyekiti?
3.Ukiwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba ni dhahiri kabisa umekuwa
ukishindwa na Yanga kupata haki zako kuhusu umiliki wa wachezaji kama
ulivyompoteza bure beki Kelvin Yondani, ulivyonyanga’anywa beki
Mnyarwanda Mbuyu Twite na ulivyompoteza winga mwenye kasi Mrisho Ngassa.
Unavyofahamika wewe ni muelewa na mchambuzi mzuri wa kanuni:-
a) Kwa nini hukuzingatia vizuri kanuni ili kufanikisha umiliki wa wachezaji hao dhidi ya watani wako wa jadi Yanga?
b) Kwa nini hukuchambua vizuri kanuni kuona Yanga ilikosea mahali katika kuwanyang’anya wachezaji hao?
c) Mbona katika kesi zote hizo ulionekana kuwa baridi sana tofauti na
nguvu zako unapopigania haki, je kulikuwa na shinikizo lolote toka
mahali fulani pazito?
4. Katika suala la Mbuyu Twite ulilia machozi ulipokuwa ukilieleza
kwa waandishi wa habari. Nini hasa kilikuliza katika sakata lote hilo?
Nini tafsiri ya machozi yako?
5. Hebu tueleze kuhusu biashara tata ya mchezaji wenu Emmanuel Okwi
wa Uganda kwa Etoile du Sael ya Tunisia. Mgogoro wa malipo uko vipi na
unaamini FIFA wanaweza wakaamua vipi kuhusu suala hilo? Je mchezaji huyo
anaweza kwenda Yanga kama inavyovumishwa sasa hivi? Ili aende klabu
nyingine mbali ya Simba na Etole du Sael utaratibu wa kwenda huko
utakuwaje?
6. Ulipoingia Simba kama Mwenyekiti mwaka 2010 uliahidi mambao kadhaa
ambapo mawili makubwa ni kuhakikisha Simba Sports Club inanufaika na
rasilimali zake kwenye mtaa wa Msimbazi yalipo makao makuu yake kwa
kuhakikisha inakuwepo mikataba halali ya wapangaji kulingana na gharama
halisi ya upangaji kwenye eneo hilo la Kariakoo na jingine ni mchakato
wa ujenzi wa uwanja wa klabu ya Simba kule Bunju. Je mmefikia wapi kwa
hayo yote mawili? Kama kuna mikwamo, nini sababu ya mikwamo hiyo?
7.Hivi karibuni ulionekana kwenye vyombo vya habari ukiwasainisha
wachezaji wawili kuichezea klabu ya Simba, mmoja ni mtanzania kutoka
Misri na mwingine toka Mtibwa Sugar. Nafahamu wewe ni mhasibu kitaaluma
kama sijakosea lakini ulionekana ukiwasainisha wachezaji hao huku kiasi
cha pesa kikiwa hapo mezani ikimaanisha ni malipo yao. Huu ni utaratibu
sahihi wa kifedha badala ya kuwalipa kwa hundi? Je wachezaji hao ni
pendekezo la kocha au ni mipango yako binafsi?
8. Simba kwa sasa ni wazi iko kwenye mgogoro baada ya wewe Mwenyekiti
kusimamishwa na kamamti ya utendaji uenyekiti ukiwa nje ya nchi. Kwa
mujibu wa katiba ya Simba, kamati ya utendaji ina mamlaka hayo? Kama
inayo, katika mazingira yapi?
9. Kwa nini TFF ilipokuagiza uitishe mkutano mkuu wa dharura ndani ya
wiki mbili kuzungumzia mgogoro huo, ulikaidi hadharani kwa kueleza kuwa
hautatekeleza hilo? Umezingatia kanuni gani kukaidi agizo hilo na kwa
nini msingewasiliana na TFF wenyewe tu badala ya kuumbuana hadharani
kupitia vyombo vya habari?
10. Nani atakuwa kocha mkuu wa Simba kati ya Mtanzania King Abdallah
Kibaden na Mkroatia Zdravko Logarusic ikizingatiwa kuna pande mbili kila
moja ikimzungumzia mmoja wa makocha hao? Nani mwenye maamuzi ya kuajiri
na kufukuza kazi kocha kwenye klabu ya Simba?
11. Una mkakati gani wa kumaliza mgogoro wa sasa wa Simba ili kurudisha umoja ndani ya klabu hiyo?
No comments:
Post a Comment