Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) akiwasalimia vijana chini ya miaka 17 kabla ya kukutana na timu ya vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa.
Mchezaji wa zamanai wa Manchester United Andy cole(wa pili kulia) akisisitiza jambo kabla ya kujumuika na vijana wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 jana - Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania.
Meya wa manispaa ya Ilala(wa pili kushoto) akikabidhi mipira iliyotolewa na Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bwana Jamali Malinzi (kushoto) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni mchezaji wa zamani wa klabu Manchester UnitedAndy Cole na Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Sunil Colaso(kulia).
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester united(Kulia) akionyesha ufundi wa kuchezea mpira mbele ya timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 jana jijini Dar es Salaam. Anayeangalia ni Meya wa Manispaa ya Ilila Jerry Slaa.
Meya wa Manispaa wa Ilala Jerry Slaa akipiga mpira katika hafla iliyoandaliwa na Airtel jana kukabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17. Anayeangalia(kushoto) ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bwana Jamal Malinzi.
========= ======= ==========
KAMPUNI
ya Airtel Tanzania imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali
katika kuendeleza michezo nchini ili kuleta ufanisi katika sekta ya
michezo.
Akizungumza kabla ya kukabidhi mipira 100 kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso alisema uwekezaji katika michezo ni mhimu hasa katika kipindi hiki amabacho Tanzania inajipanga kushiriki katika mashindano ya kikanda na kimataifa.
“Airtel Tanzania tunakabidhi mipira 100 kwa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 kama sehemu ya juhudi zetu kusaidia maendeleo ya michezo.
“Tutaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha nchi inapata mabalozi wa kutuwakilisha vizuri katika mashindano ya kimataifa” alisema.
Colaso alisema mwaka 2011 kampuni yake kwa makusudi ilianzisha Airtel Rising Stars ikiwa ni mpango wa kuvumubua na kuendeleza vipaji kwa vijana wadogo kutoka ngazi ya chini ili kuwapeleka ngazi za kimataifa.
Wakati wa hafla hiyo, mkongwe wa klabu ya Manchester United Andy Cole aliwaasa vijana hao chini ya miaka 17 kuongeza bidii ili kutimiza ndoto zao za kucheza kwenye timu kubwa duniani.
“Nimeona vipaji vingi Tanzania. Wachezaji wanaweza kabisa kuchezea klabu kubwa kama wataongeza bidii katika mazoezi yao. Naomba nichukue nafasi kuwakumbusha wachezaji chini ya miaka 17 kuwa na nidhamu si ndani tu ya uwanja bali na nje ya uwanja kwani hiyo ndio nguzo ya mafanikio” Alisema.
Nae Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa aliwashukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa juhudi zake endelevu kusaidia michezo na kutoa wito kwa makapuni mengine kuiga mfano wa Airtel katika kusaidia michezo.
“Tunahitaji nguvu za pamoja kati ya sekta binafsi na umma kama kweli tunataka maendeleo katika michezo. Nawashukuru sana Airtel kwa mchango wao katika michezo, niwaombe makampuni mengine waige mfano huu katika kusaidia juhudi za Serikali kuendeleza michezo

Ally Kashushu AKNOWLEDGED
No comments:
Post a Comment