Hivi karibuni nilipata kuskia kocha wa klabu moja hapa nchini akisema wachezaji wa Tanzania hawafundishki watu walio wengi walimtukana kocha Yule na kusema kuwa amewadharau wachezaji wa kitanzania hawafundishiki mimi sasa nanyanyua kinywa na ninasema ndio hawafundishi nina amini hawakumuelewa mkufunzi huyu napengine sio wachezaji wa kitanzania hata raia ambao sio wachezaji nini maana ya kutofundishika ?
Maana yake kutofuata maagizo ya
mwalimu na kufanya yale ambao hukupewa hii ndio maana ya kutofundishika ndio
maana Hata klabu mbili za simba na yanga kubadili makocha kila siku iendayo kwa
mungu hii ndio maana ya kutofundishika wengi
walikasilika hata wadau mbalimbali wa soka wakisema kocha Yule kawakosea
heshima wachezaji wa kitanzania Binafsi yangu ninasema wala hakuwakosea heshima
alisema ukweli tatizo ni kutokukubali ukweli .
Mara kadhaa Tanzania imeshindwa
kufanya vizuri sio klabu wala timu ya taifa hata wakati makocha wa kigeni
wamekuwa wa kibadili wachezaji mara kwa mara hii inaonyesha kuwa hata makocha
wamekuwa wakishindwa kupata safu nzuri ya wachezaji kwa sababu ya uelewa mdogo
wa wachezaji wa kitanzania na timu chache sana ambazo huwa zinaweza kuka na
wakufunzi kwa muda mrefu na timu zote ambazo zimekuwa zikibadili makocha kila
kukicha hii ina maana ya kuwa hawafundishi kwani huwezi kubadili makocha kama unafanikiwa
haina sababu.
kocha wa kigeni toka ulaya ambaye amewahi
kukaa kwenye klabu kwa zaidi ya miaka mitano hakuna .
Na kutokana malezi hafifu ya watoto
wa kitanzania ni vigumu sana kupata mchezaji anayeweza kufundishika ni vigumu
kwani katika mazingira ya kitanzania baadhi ya wachezaji wa kitanzania hawajui
hata kiingereza kwani Kiswahili tun kinawapa shida na matokea yake hushia
kuzungumza Kiswahili cha mtaani na walio wengi hawakukaa darasani kukaa na
mwalimu anae zungumza kingereza ni ndoto
kuelewa hakika na kubaliana na mkufunzi huyu kwani uelewa wao hata katika
masomo ya shuleni ni mdogo ndio maan sifuri ni nyingi darasa saba kidato cha
nne hadi kidato cha sita na walio wengi hujaribu hata kufoji matokeo ili waende
chuo kikuu sasa tukiambiwa hatufundishiki mtakataaa .
Tunaweza kuweka vigezo vya kutafuta kocha lakini lazima
tujiulize je tuna aina ya wachezaji wa mpira wa miguu wanaoweza kuchezeshwa na
kocha mpya je itawezekana vipi jambo la msingi ambalo watanzania wanatakiwa
kuelewa mfumo mzima wa kielimu Tanzania auwiani na wanafunzi kila waziri wa elimu anayekuja
kuongoza wizara anakuja na mtazamo mpya je mnafikiri ni rahisi kuona soka
yakufundishwa kwa tanzania kila siku tunalia jinsi ya kutafuta wachezaji jambo ambalo limekuwa ndoto kushiriki
michuano ya vijana na tumeishia kudanganya umri .
sasa maana ya kutofundishika ni
kudanganya umri kwa sababu kama umeshindwa kugundua umri sahihi au kupindisha
sheria kimakusudi huko ni kutofundishika jamani .
Watanzania wenzangu lazima tutafakari
kabla ya kuanza kutuhumu mtu anapotoa kauli yake ya watu kutofundishika .
No comments:
Post a Comment