Klabu za Yanga na Simba zimeagizwa kulipa jumla ya sh.
milioni 25 kutokana na uharibifu wa viti na vurugu zilizofanywa na washabiki
wao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga italipa sh. milioni 15 ambayo ni gharama ya
uharibifu wa viti uliofanywa na washabiki kwenye mechi hiyo. Pia imepigwa faini
ya sh. milioni tano kutokana na vurugu za washabiki wake. Nayo Simba imepigwa
faini ya sh. milioni tano kutokana na washabiki wake kuhusika katika vurugu
hizo.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha dharura
kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Tunatoa onyo kwa washabiki wa mpira wa miguu
kujiepusha na vurugu viwanjani ikiwemo uharibifu wa miundombinu mbalimbali ya
viwanja ikiwepo viti, na tutachukua hatua kali zaidi kwa klabu na washabiki
wake iwapo vitendo hivyo vitajitokeza tena.
No comments:
Post a Comment