HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

27 October 2012

ICE CREAM ZASHINDWA KUHIMILI MISITU YA MSIMBAZI YAKUTANA NA JOTO KALI


Emanuel Okwi akikimbia huku akishangilia bao lake la kwanza alilofunga katika mchezo wa ligi kuu ya premier tanzania dhidi ya Azam fc mchezo iliokwisha kwa ushindi mabao matatu kwa moja kwa simba kuibuka na ushindi .


Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akiukimbilia mpira huku beki Ibrahim Shikanda wa Azam fc naye akiuwahi kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa Taifa Leo katika uwanja wa taifa  na simba kushinda mabao 3-1.


Mshambuliaji wa chipukizi wa Simba Ramadhan Singano wa Simba akiwatoka beki wa Azam Sahm Nuhu kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Taifa leo hii simba imeshinda mabao matatu kwa moja


Yanga leo imeshika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuifunga Oljoro JKT bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Yanga sasa itakuwa na pointi 20 wakati simba inayoongoza ligi hiyo imefikisha pointi 22. Azam pointi 18.

Kwa ushindi huo, Yanga imetimiza pointi 17, baada ya kucheza mechi 10 na inaendelea kusimama katia nafasi ya tatu.

Mechi nyingine za ligi hiyo leo ni kati ya African Lyon na Kagera Sugar Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, Mgambo JKT na Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting dhidi ya Polisi Morogoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo miwili kati ya JKT Ruvu na Coastal Union Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Toto Africans dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 


No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers