Karibu mpenzi wa kurasa ya yangu kwa
heshima na taadhima leo tena nakuelezea kuhusu soka ya Tanzania .
Najua Tanzania ni ambayo mungu
kaipenda kiasi kwamba haijawahi kutokea vita ya kutoewana kati ya jamii ya
kitanzania tofauti na mataifa mengine ya afrika vita pekee ilipiganwa wakati wa
kumtoa Idd Amin rais wa Uganda ambayo Tanzania ilishinda vita hiyo la hasha
usininukuu vibaya kuwa nataka tupigane hapana.
Kunatofauti kubwa sana ya wachezaji
kutoka afrika magharibi na afrika mashariki
siku zote huwa ninaamini ukiona mchezaji kutoka afrika Magharibi kaja
Tanzania kucheza soka huyo sio mchezaji ni skrepa lakini ngoja nije kwenye
alama ya msingi.
Wachezaji wetu wa Tanzania
wanashindwa kucheza mpira ulaya kwa sababu moja kuu nayo lelemama sio wachezaji
wote wa kiafrika ambao wamepita kwenye shule za soka lakini wakafanikiwa
kucheza soka, wengi wa wachezaji hawa ni walikubari kulala hata kwenye vituo
vya mabasi huko ulaya walikubali hata kufagia barabara za ulaya na wengine kutukanika
kufanya hata kazi za kukosha vyombo lakini ukiiosha vyombo afrika utaoneka huna
maana chembe.
Wapo wachezaji wa kitanzania ambao
wamekwenda ulaya na wameshindwa kusakata kabumbu la ulaya kwa kusingizia ujira
mdogo na wengine wakipelekwa hata vikosi vya tatu kufanyiwa marewkebisho lakini
wakawaona wazungu wapumbavu sasa kati yao na wazungu nani mpumbavu.
Kikubwa soka ya ulaya bila kujali
ligi ni ya nchi gani huwa sio lelemama kabisa kwani mchezaji lazima ukubali
kufa lakini sio kwa wachezaji wa kitanzania
ambao wengine wanapata bahati ya kucheza ulaya lakini hawaonyeshi uwezo na
matokeo yake huishia kurejea kucheza ligi ya nyumbani ,mchezaji yotote Yule
kutoka Tanzania ambaye amekwenda ulaya kucheza akashindwa kucheza huko au
kacheza lakini kaamua kurudi nyumbani huyo ameshindwa maisha .
Wapo wachezaji wengi wakitanzania
ambao wamecheza nchi za ulaya na America ya kaskazini ambapo ligi zao sio bora
kama zile za ulaya lakini wameshindwa kutokana na kushindwa kukomaa na hari ya
kimaisha wengi wamekuwa wakitaka mishahara minono tofauti na uwezo wao je
unadhani ni rahisi ulaya unalipwa kutoka na kazi unayofanya na ubishi wako
kiwanjani.
Wachezaji wanatakiwa kuacha mchezo
kiwanjani na sio kuwaza starehe za nje ya kiwanja ambazo hazina maana .
No comments:
Post a Comment