Moja kati ya mambo ya
msingi ambayo watanzania wengi wanataka
katika soka ya Tanzania ni ushindi bila
kujari unapatikana vp ? Mara nyingi huwa tunasingizia kuwa hatuna maandalizi ya
kutosha ya kupambana na timu pinzani je
tunahijati maandalizi ya aina gani ili tuweze kufanikiwa angalau kucheza
michuano ya kimataifa.
Katika kulitazama
hili nimekaa na baadhi ya makocha wa Tanzania ili kuweza kujua tatizo nini ni ?
hasa kiasi cha Tanzania kushindwa kufnya vizuri sio katika soka tu bari katika
michezo yote Tanzania .
Moja kati ya majibu
ya kimsingi ambayo nimeyapata katika tafiti zangu nilizo fanya, kuu kuliko
yote ni kuwa wachezaji wa Tanzania hawajui ABCD za mpira wa miguu kiasi ambacho
wachezaji wengi wa kitanzania wanashindwa hata kufanya majaribio nje ya nchi.
Ni vigumu mmno
kufanikiwa hata kama tukaleta kocha kutoka Ujerumani au uholanzi naam wengi
wetu tumekuwa tukiweka siasa ya kuwa hakuna kisichowezekana katika mpira
wa miguu lakini ukitazama kiuhalisia
wachezaji wa kitanzania na makocha wetu wa leo hawajui soka la kiufundi kabisa
na kuna makocha wa chache ambao wanajua kufundisha soka la kiufundi lakini
wamekuwa hawapewi nafasi kwani nabii siku zote huwa hakubaliki kwao
.
Kwa hari ilivyo sasa
ni lazima tupeleke makocha wetu nje ,wakasome na waje kufundisha soka ndani ya
nchi yetu na wakatembee katika mashule ya ili waweze kutoa elimu ya soka katika
shule zao bila kufanya hivyo tutakuwa tunampigia mbuzi gitaa kila mwaka .
Lakini poulsen
anaondoka huku akisema kuwa wachezaji wa kitanzania sio professional wa
kucheza mpira wa miguu kwani hawakuandaliwa kufanya hivyo ni wavivu wa kula na
vile vile wanacheza mechi wakiwa wamefunga
je unadhani ni rahisi kucheza soka kwa mchezaji ambaye anacheza soka ya
ridhaa professional ligi ya Tanzania ni professional lakini wachezaji hawana
matendo ya kiprofesional
Bila kuelewa ABCD za
mpira wa miguu itamchukua mchezaji mmoja wa kiatanzania Miaka mia moja na
themanini kuwa sawa na wachezaji wanaocheza ligi daraja la nne ulaya sababu
hawajui ABCD za mpira miguu na najua unaaniuliza zimnapatikana wapi ABCD
za soka timu za Tanzania zinatakiwa kuwa shule za soka ambazo zitakuwa
maalum mtoto afundishwe akiwa mdogo na Elimu ya dunia waijue wakiwa tangu
watoto .
No comments:
Post a Comment