Timu ya soka ya Taifa ya Ivory coast imewatoa kimasomaso waafrika mara baada ya kuwabamiza watengeneza magari kutoka japan kwa mabao mawili kwa moja kwenye mchezo wa Kundi c ambao ilikuwa mechi ya mwisho kwa saa za brazil mechi ilichezwa usiku wa manane lakini ujapan ilikuwa majira ya saa nne asubuhi na afrika mashariki ilikuwa saa kumi alfajiri
Japan ndio walikuwa wa kwanza kupata goli katika dakika ya 16 goli lilofungwa na mchezaji mahiri wa japana Honda hadi nusu ya kwanza ya mchezo Ivory coast ilikuwa ipo nyuma kwa bao kwa sifuri .
Kipindi cha pili kilikuwa cha waafrika kutoka na raha kwa mara ya kwanza msimu huu pale Wifred bony aliposawazisha kwa mpira wa kichwa akiunganisha krosi toka wingi ya kushoto na baadae Gervinho kufunga bao la pili na kuhitimisha Rekodi ya wajapan kutofungwa na timu za afrika .
Katika mechi za awali Uingereza ilikung'utwa na italia mbili moja wakati
Costa rica ikailaza Uruguay tatu moja na Colombia ikaizaba Ugiriki Tatu sifuri
- Mechi za leo
- Switzerland v Ecuador 17:00
- France v Honduras 20:00
- Argentina v Bos-Herce 23:00
- Iran v Nigeria 20:00
No comments:
Post a Comment