Rais aliyemaliza muda wake Simba Ismail Aden Rage akabidhi nyaraka na mali ya klabu kwa Rais mpya wa klabu hiyo Evance Aveva |
Aliyekuwa
mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage hii leo amakabidhi
ofisi kwa uongozi mpya wa klabu hiyo ambao unaongozwa na Evance
Elieza Aveva mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchaguzi mkuu
uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.
Ismail
Aden Rage amefanya makabidhiano hayo ya ofisi kwenye makao makuu ya
klabu ya Simba ambapo amekabidhi nyaraka mbalimbali za kiutendaji wa
klabu hiyo kongwe hapa nchini.
Hata
hivyo rage ameushauri uongozi wa Evance Aveva kufuata taratibu ambazo
alizitumia wakati wa uongozi wake wa kipindi cha miaka minne hususana
katika suala la vyanzo vya fedha.
Kitu
kingine ambacho Rage amekigusia ni kumtaka Rais wa klabu ya Simba
Evance Aveva kutatua kwa kutumia busara suala la wanachama wa klabu
hiyo waliokwenda mahakani kwa lengo la kuzuia uchaguzi.
Katika
hali ya kushangaza Ismail Aden rage akazungumzia na kukabidhi nyaraka
zinazoonyesha uhamisho wa mshambuliaji Emmenuel Okwi ambae aliuzwa na
klabu ya Simba huko ndhini Tunisia kwenye klabu ya Etue Du Sahel.
Baada
ya kukabidhiwa nyaraka za klabu ya simba Rais mpya Evance Aveva
alimshukuru Ismail Aden Rage kwa niaba ya kamati yake ya utandaji
huku akimtaka kutojiweka mbali mba wao kutokana na kuona bado kuna
hitajiko la nguvu zake ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi.
No comments:
Post a Comment