Kocha na Mkufunzi wa makocha Tanzania Rogasian Kaijage amesema kuwa wachezaji walioshiriki michuano ya Rolingstone bado hajajua hatima yao itakuwa wapi na kubwa zaidi amesema kuna Udanganyifu mkubwa wa wachezaji Kudanganya Umri kwani wapo wachezaji ambao yeye mwenyewe Binafsi amekiri kuwatambua na kusema wanacheza soka kwa Muda Mrefu.
Michuano hiyo hutumika kwa kuibua vipaji ambapo safari yamefanyika katika mkoa wa Dar Es Salaam kwani mara kadhaa yamekuwa yakifanyika mkoani Arusha na Timu ya Vijana ya Azam kutwa Ubingwa huo
wa Rolling Stone 2014 baada ya kuichapa magoli 2-0 timu ya JWTZ Twalipo
Academy katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa karume Jijini Dar es salaam.
Magoli yaliyofungwa na Jamil Mchaulo Baloteli dk4 na Adam Omar Soba dk88 yametosha kuipa ushindi Azam Academy .
No comments:
Post a Comment