Mchezaji wa Zamani wa Klabu ya soka ya Real Madrid na Timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa Christian Lali Karembeu ameomba mechi ya Marejeano kati ya Timu ya soka Ya magwiji wa Real Madrid na Timu ya soka ya Mastaa wa Tanzania baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa kirafiki ulichezwa kwenye uwanja wa taifa huku ukishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Khalfan Mrisho kikwete .
Mchezo huo uliiisha kwa ushindi wa Magwiji wa Real madrid wa mabao matatu kwa moja mara Baada ya kumalizika kwa Mchezo huo Dunia ya Michezo ilipata nafasi ya Kuzungumza kwa kifupi na Nyota huyo na alisema.
CHEZESHA
Ilikuwa ni mechi Nzuri na wamecheza Vizuri sana walikuwa na uwezo mzuri wa kukimbia kiwanjani waliweza kubana nafasi na walitupa wakati mgumu matumaini yetu tunaweza kuja kucheza nao tena mechi hapa .
Aidha wachezaji wengine waliokuwepo kwenye kikosi cha Real Madrid ni Luis Figo,Fabio Canavaro,Ruben dela Red aliyefunga mabao matatu na pamoja na Fernando.
No comments:
Post a Comment