Timu ya taifa inaangaika utafikiri
mgonjwa ambaye anaumwa maradhi yasiponyeka na Muda wowote anasubiriwa Israel
Mtoa Roho tu Aje aitimishe safari ili iingie kaburini yanaweza kuwa maneno
makali sana kwenye macho yako kuyasoma lakini hii ndivyo hari ilivyo kwani sasa
unaweza kujionea wazi labda niulize swari ni kocha au wachezaji Ndio wenye matatizo kwani ni
mchezaji gani ambaye hakuwemo Tangu wakati wa Maximo ukianzia Golini mpaka
wafungaji?
Kwanini Mariga ,Wanyama,Oriech ,Origi
wanacheza soka ulaya kwanini Kapombe kashindwa ufaransa? Kwanini Haruna Moshi
kashindwa Sweden? ,Kwanini Ngasa kashindwa Uingereza? Kwanini nizar Khalfan Karudi
Kutoka Canada? kwanini tunakimbilia Arabuni kila siku Kuna tatizo Gani ?
Mimi leo nakueleza Ukweli wachezaji
wa Tanzania Uwezo wao ni mdogo Tangu maximo alipochukua Timu aliita wachezaji
wangapi Timu ya Taifa Ukihesabu sasa wanaweza kufika hata Hamsini lakini Bila
bila Mchezaji wa Mpira wa Miguu anatunza kiwango cha soka kwa kiwango chake
mwenyewe na sio timu mwaka 2002 Uingereza ilikuwa kundi Moja na Sweden
wachezaji wa Sweden walikuwa wakicheza katika ligi Daraja la pili uingereza
unadhani kwanini waliweza kuisimamisha uingereza ni kutokana na uwezo sina
maana ya kufananisha hapana najalibu kukupa mfano tu.
Wachezaji wengi watanzania Wamefeli shule !wengi Darasa la saba na kidato cha Nne je watamuelewa kocha kama kuna mchezaji ambaye
ana Digrii anyooshe Mkono sidhani kama kuna mtu atanyoosha mkono kiukweli
wachezaji watanzania ni wabishi kuelekea wao wenyewe ni makocha kuwakacha
walimu lakini Jamani Hivi Tanzania hakuna kocha ? asilimia kubwa ya Timu za
zote Zinafundshwa na wazawa ukiacha timu Kubwa Mbeya city ambaye alikuwa
akitishia usalama wa watu inafundishwa na Mzawa Juma Mwambusi Lazima tutazame
ni kweli Maximo hajui kufundisha,Jan na Kim hawajui kufundisha Mart naye hajui
kufundisha ?
Ukiacha Darasa moja linabadilishwa
walimu kila siku wanafunzi wale wale juaeni kuwa mnampigia Mbuzi gitaa .
Malinzi pole sana naona una kazi kuliko
kocha ukitazama huku makocha inaonekana huna waamuzi huna wachezaji short kozi
Sijui kama timu unayo? Miundo mbinu je ?
Labda tuulize swali dogo tunataka
kitu gani kwasababu mipango Midogo tumeshindwa kwa mara nyingine tena mipango
ya Muda Mfupi imechemka kwenda Afcon ,Inashindwa kutwaa chalenji,inashindwa
kwenda kombe la Dunia je tunataka mpango wa Muda mfupi kwa ajiri ya kitu gani
ni nchi gani imefanikiwa kutwaa au kushiriki michuano mikubwa kwa mipango
mifupi ?kwanini tusijaribu wa Muda Mrefu ?
Hivi ni kweli timu ya Kenya inatuzidi
kiwango au ni uzembe wa wachezaji wetu tu
No comments:
Post a Comment