Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza
kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16
mwaka huu jijini Mbabane.
Akizungumza Dar es Salaam, leo (Novemba
5 mwaka huu), Nooij alisema kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 10 mwaka huu
saa 6 mchana kwenye hoteli ya Accomondia, na siku hiyo hiyo jioni kitafanya
mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
Novemba 11 mwaka huu, Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwenda Afrika Kusini
ambapo itaweka kambi ya siku mbili kabla ya kuondoka Novemba 13 mwaka huu
kwenda Swaziland.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho
ni makipa Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar
Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan
Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua
(Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe
(Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto
Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al
Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO,
Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon
Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).
No comments:
Post a Comment