HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

11 December 2012

240 Zampeleka Ngasa El Mereikh Simba, Azam zalamba Milioni 80 kila moja, Ngassa naye alamba mil 80 na mshahara mnono


Klabu ya soka ya El Meriekh ya Sudan imetoa dola 100,000 sawa na  (shs 160 million) kuzilipa klabu za Azam FC na Simba SC ili kuondoa mgogoro wa usajili wa mchezaji Mrisho Ngassa.

Awali El Meriekh ililipa Dola za Kimarekani 75,000 sawa na  (shs million 120) kwa klabu ya Azam FC pekee kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyo na kuzua mtafaruku mkubwa dhidi ya klabu ya Simba na kuamua kuweka pingamizi katika Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), CAF na Fifa.

Simba ilidai kuwa Ngassa ni mchezaji wao halali kutokana na ukweli kuwa ilimnunua kwa shs milioni 25 zilizotakiwa na Azam FC na kumlipa stahiki zake zote kwa mujibu wa mkataba huo.

Pamoja na kupata upinzani mkubwa kutoka kwa timu ya Azam FC kutokana na ukweli kuwa Ngassa alikuwa akiichezea Simba kwa mkopo, Simba iling’ang’ania na msimamo wake na kupeleka suala hilo mbele ya vyombo vya sheria vya TFF ili kupata haki yake.

TFF ilishauri klabu hizo kukaa meza  moja ili kuona kuwa wanaondoa utata huo, jambo ambalo lilifanyika Jumatatu na Jumanne na kufikia muafaka huo na El Meriekh kulipa fedha zaidi na kumfanya mchezaji huyo kusajiliwa kwa Dola za Kimarekani 150,000 sawa  na  (Milioni 240 ukijumuisha Dola za Kimarekani 50,000 atakazolipwa Ngassa na El Meriekh) na kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa kitita hicho hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala amesema kuwa wamefarijika sana na makubaliano hayo na wao kutoa kipingamizi cha Ngassa kwenda kufanyiwa vipimo vya afya mjini Khartoum kabla ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo.

Mtawala aliongeza  kuwa hayo ni matunda ya kujadili mambo katika meza moja na wala si kwa kutimia vyombo vya habari kwani wao walijua haki yao ipo wapi.

Afisa Habari wa Azam FC, Jaffer Idd alithibitisha makubaliano hayo na kusema uongozi wa klabu hiyo chini ya makamu mwenyekiti, Shan Christoms na Twalib Suleiman aliyemwakilisha katibu mkuu, Nassoro Idrissa ndiyo waliofikia makubaliano hayo.

Simba SC iliwakilishwa na Mtawala na Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange Kaburu “Ni faraja kwetu kufikia maamuzi haya, lengo ni kumfanya Ngassa atimize ndoto yake katika soka na wala si vinginevyo,” aliongeza  Idd.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers