HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

7 December 2012

KELELE ZAANZA JIJI LA MANCHSTER !!!!!


Manchester City Na  Manchester United  Wataonyeshana umwamba kesho jumapili katika uwanja wa ETIHAD  ambapo mechi hiyo inaweza kutoa Taswira ya nani anaweza kutwaa au nani anaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa nchi hiyo .

Roberto Mancini's   alishuhudia timu yake ikipata ushindi katika mechi zote mbili msimu uliopita baada ya kushinda mabao sita kwa moja katika uwanja wa old traford na baadaye kushindi goli moja sifuri katika uwanja wa ETIHAD na  kushinda ubingwa kwa staili  ya aina yake siku ya mwsisho ya ligi kumalizika.

City wameanza vizuri msimu huu katika utetezi wa lgi ya uingereza na hawajafungwa katika mechi 15 walicheza lakini united ndio wanashikiria faida ya uongozi wa alama tatu katika mechi   zilizo pita 
Tayari kumekuwa na minong'ono kuwa Timu hizo mbili ndizo zinazowania ubingwa ,
huku timu nyingine zikiwa zinajitahidi kutafauta angalau uimara wa kushinda kila mechi 
,Kukutana kwa Timu hizi mbili   City na  United kunaweza kuthibitisha hilo katika uongozi wa ligi 

Vile vile kumekuwa na mazungumzo kuhusu kutolewa mapema kwa City katika ligi ya mabingwa bara la ulaya ambapo kunaweza kumfanya Mancni kuwa na kazi moja tu ya kuwania ubingwa wa uingereza kwani ndio kibarua pekee alichokua nacho 
 huku mwenzake akiwa na vibarua vingine.


Ushiriki wa City' katika ligi ya mabingwa barani ulaya uliishia kwa mikononi mwa  Borussia Dortmund baada ya kufungwa bao moja sifuri katika ya wiki wakati tayari walikwisha kwenda sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Everton baada ya kuonyesha kiwango ambacho sio kizuri na kisichovutia 
wakati United walikung'utwa bao moja  ugenini dhidi 
 CFR Cluj siku ya jumatano japokuwa tayari walikwisha fuzu hatua inayofuata ya ligi ya mabingwa bara la ulaya jambo lililomfanya   Sir Alex Ferguson kutokupanga kikosi chake cha kwanza  

Mashetani wekundu waliifunga Reading 4-3 wiki iliyopita na kuishusha city  na ilikuwa ni  mechi nyingine ambayo united ilitoka nyuma na kushinda mechi hiyo japokuwa Ferguson akufurahishwa na namna safu yake ya ulinzi ilivyocheza.

Ferguson atakuwa anahitaji  uangalifu wa  hari ya juu kwa kupambana na timu ambayo ina safu nzuri ya ulinzi ambayo ndiyo bora zaidi  hadi sasa,
na mwenyewe   Ferguson amsema  kamawatashinda  utakuwa ni ushindi mzuri zaidi kuupata tena nyumbani kwa ndugu zao Manchester city ndani ya miaka miwili .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers