HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

27 June 2014

ALGERIA YALETA HESHIMA AFRIKA YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA


 Algeria imeunga na Nigeria katika hatua ya kumi na sita katika michuano ya Kombe la Dunia mara baada ya kutoka Sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Urusi katika mchezo wa Kundi H Urusi ndio waliokuwa wakwanza kupata goli lilofungwa na Kokorin katika dakika ya sita akiunganisha mpira wa krosi wingi ya kushoto na kumwacha mlinda mlango wa Algeria Rais mdomo wazi lakini Dakika ya sitini na sita  SLIMANI alisawazisha goli akiunganisha mpira wa kichwa baada ya kupingwa mpira wa Adhabu Dogo upande wa kulia mwa Lango la Urusi .

Algeria  inaifanya bara la afrika kuingiaza timu mbili kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe la Duania mara kadhaa timu za afrika zimekuwa zikiingia raundi ya mtoano ambapo ni timu mmoja tu ambapo hufanikiwa kuingia hadi robo fainali .
katika hatua inafuata Algeria itapambana na Ujerumani ambapo mwaka 1982 Algeria ndio ilikuwa timu ya kwanza kuifunga ujerumani katika michuano ya kombe la Dunia .
Mchezo huo utachezwa siku ya jumatatu ambapo siku hiyo hiyo wawakilishi wengine kutoka afrika Nigeria itakumbana na Mabingwa Dunia mwaka 1998 ufaransa timu nyingine za afrika zilizo fungasha virago ni ghana ambao wametandikwa mbili sifuri dhidi ya ureno wakati ivory wakitandikwa mbili sifuri dhidi Ugiriki 
wakati Cameroun wakichapwa nne sifuri na wafalme wa samba duniani Brazil

1 comment:

  1. Matokeo mengine ya timu za Afrika hayako sawa kaka, umetupotosha au umepotosha wasioangalia mechi husika.

    ReplyDelete

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers