Kiungo wa klabu ya LA Galax ya nchini Marekani ambae anaichezea klabu ya AC Milan ya nchini Italia kwa mkopo David Beckham hii leo amekabidhi kitabu chenye kurasa 1,752 ambacho huenda kikaishurutisha FIFA kuipa nafasi Uingereza kuandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ama 2022.Beckham ambae ni mmoja wa mabalozi wanaoipigia debe Uingereza ili iweze kupewa nafasi ya kuandaa fainali hizo mwaka 2018 ama 2022, amekabidhi kitabu hicho kwa raisi wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Sepp Blatter kwenye ofisi za shirikisho hilo huko mjini Zurich nchini Uswiz
No comments:
Post a Comment