Msimu wa michuano ya kuwani ubingwa wa ligi ya Ulaya kwa mwaka 2009-10 hii leo unafikia tamati kwa mchezo wa fainali kuunguruma huko nchini Ujerumani mjini Humburg.Mchezo huo wa fainali utashuhudia klabu ya Fulham ya nchini Uingereza ikipepetana vilivyo na klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania.Mchezo huo tayari umeshaanza kumtia washa washa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uruguay na klabu ya Atletico Madrid Diego Forlan ambae amewataka wachezaji wenzake kuwa makini na wapinzani wao ambao msimu huu wameonekana kuwa moto wa kuotea mbali kwenye michuano hiyo.Amesema endapo watashindwa kuwakabili ipasavyo huenda wakashindwa kutimiza ndoto zao za kuwa mabingwa wa ligi ya ulaya ambazo kila leo wamekua akiziota.Fulham walifanikiwa kuingia kwenye hatua ya fainali baada ya kuwaondoa wenyeji wa mchezo wa leo wa fainali Humburg SV ambao wataushuhudia mchezo wakiwa jukwaani, huku Atletico Madrid walifanikiwa kufika kwenye hatua hiyo baada ya kuwaondosha Liverpool.
No comments:
Post a Comment