Kocha wa timu ya SIMBA PATRCK PHIRI kulia akiwa ameongoza na mchezaji wa timu hiyo JUMA JABU kushoto pamoja na meneja wa timu hiyo INOCENT NJOVU katikati.
Wachezaji ROBERT SSENTONGO aliyekuwa akichezea timu ya AFRICA LYON na ABDULRAHIM HUMUD aliyekuwa akichezea MTIBWA SUGAR msimu uliopita wamejiunga na kikosi cha SIMBA ambacho kimeondoka nchini leo kwenda RWANDA kushiriki mashindano ya KAGAME kwa vilabu.
Akizungumza wakati timu hiyo ikiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere, kiungo ABDULRAHIM HUMUD ambaye anachezea pia timu ya taifa , TAIFA STARS , amesema anajisikia faraja kuchezea klabu kama ya SIMBA haswa katika mashindano hayo na mengineyo.
Aidha, Meneja wa timu ya SIMBA, INNOCENT NJOVU alithibitishi kuwa mchezaji ROBERT SSNTONGO ameruhusiwa kuchezea timu hiyo akitoka AFRICA LYON
Mashindano kombe la Kagame yanaaza rasmi kesho huko RWANDA, ambapo katika mchezo wa ufunguzi kutakuwa na mchezo kati ya wenyeji APR ya RWANDA ambayo itacheza na VITALO ya BURUNDI.
Wakati SIMBA wakiwa katika kundi la C watacheza na SOFAPAKA ya KENYA, mchezo utakaochezwa keshokutwa. Habari kwa hisani ya
thanks jannejonh blog
No comments:
Post a Comment