Ubingwa wa Ngumi za Kulipwa wa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati ulianzishwa mwaka 1983 katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
Mpaka
kufikia wakati huo (1983) ni nchi ya Tanzania peke yake iliyokuwa
imeshaanzisha ngumi za kulipwa katika ardhi yake ambapo Kenya na Uganda
zilikuwa bado hazijaanzisha ngumi za kulipwa nchini mwao japokuwa
zilikuwa na mabondia kadhaa waliokuwa wanacheza ngumi za kulipwa katika
nchi za Ulaya na Asia.
Mabondia
wa Kenya waliokuwa wanacheza ngumi za kulipwa nje ya nchi yao wakati
huo walikuwa ni pamoja na Steven Muchoki na mdoho wake Michael Irungu
waliokuwa wanapigana ngumi nchini Denmark chini ya Promota maarufu
Mogens Palle. Mabondia
wengine wa Kenya waliokuwa wanapigana ngumi za kulipwa nje ya Kenya
walikuwa ni pamoja na Modesti Napunyi Oduor, Isayah Ikoni na Philip
Warwinge waliokuwa wanazipiga nchini Japan.
Aidha
mabondia wa Uganda waliokuwa wanacheza ngumi nje ya nchi yao
waliongozwa na Ayub Kalule, John Odhiambo, Mustapha Waisaja, John Mugabi
(The Beast), John Rubin Byaruhanga na Cuban Businge ambao wote pia
walikuwa chini ya promota maarufu Mogens Palle wa Denmark.
Kwa
upande Tanzania bondia pekee aliyekuwa anacheza ngumi za kukipwa nje ya
nchi wakati huo alikuwa Gerald Isaac (Tanzania’s Devil kama wapenzi wa
ngumi na vyombo vya habari vya Marekani walivyokuwa wanamwita kwa ajili
ya ukali wake kwenye masumbwi ulingoni) aliyekuwa anazichapa nchini
Marekani.
Tarehe
18 mwezi wa Juni liliandaliwa pambano la kwanza la aina yake kwa
ubingwa mpya kabisa wa Afrika ya Mashariki na Kati lililofanyika katika
ukumbi wa mikutano ya kimataifa jijini Nairobi (Kenyatta International
Conference Center, KICC).
Waandaji
wa mpambano huo walikuwa ni pamoja na DS Njoroge wa kampuni maarufu ya
ngumi wakati huo DS Boxing Promotions ya jijini Nairobi nchini Kenya,
Joe Akech ambaye wakati huo alikuwa ndiye Meneja Mkuu wa Kanda wa
shirika la ndege la Marekani, Pan American Airlines (Pan Am) na David
Attan na mkewe Linda Brown Attan wa kampuni ya Davlin Boxing Promotions
ambaye baadaye alikuja kuwa Promoter wa bondia Onesmo Ngowi. Naye Joe
Akechi alikuja kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Kenya
(KPBC) na Meya wa Jiji la Nairobi.
Mpambamno
huo wa kugombea mkanda wa Bantamweight uliwakutanisha mabondia wawili
ambao walikuwa wanatamba sana katika nchi zao katika miaka ya 1980!.
Bondia Onesmo Alfred Ngowi (Piston Mover) wa Tanzania alikuwa ameshawapiga mabondiawote
waliokuwa tishio kwenye uzito wake wa bantamweight wakiwa ni pamoja na
Musa Mwabata, Sasi Sarungi, Ali Mohammed, Antoni Nyembela, Pius
Lwandalla na David Migeke.
Kwa
upande wa Kenya Modest Napunyi Oduor (Babaa) alikuwa ndiye bondia
aliyekuwa anatamba sana kwa wakati huo na ndio tu alikuwa anatokea
nchini Japan alikokuwa anapigana ngumi za kulipwa.
Wawili
hao (Ngowi na Oduor) walikutana katika mpambano wa kwanza kabisa wa
Afrika ya Mashariki na Kati tarehe 18 Juni 1983 katika ukumbi wa
Kenyatta International Conference Center (KICC) kouombea mkanda wa
kwanza wa Afrika ya Mashariki na Kati.
Katika
mpambano huo mabondia wengine toka Kenya (Steven Muchoki, Athumani, na
Michael Irungu) Uganda (Cuban Businge) Tanzania (Clement Chacha,
Emmanuel Kimaro na Fidel Haynes) nao walipanda ulingoni kusindikiza
pambano hilo la kihistoria ambalo lilianzisha ngumi za kulipwa katika
nchi za Kenya na Uganda kwa mara ya kwanza!
Refarii
wa mpambano huu wa ubingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati alikuwa
Emmanuel Mlundwa toka Tanzania wakati huo akiwa ndiye Rais wa Boxing
Union of Tanzania (BUT) iliyokuja kubadili jina na kuwa Kamisheni ya
Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) mwaka 2000!
Miaka
21 baadaye mwaka 2004 Kamisheni za Ngumi za Kulipwa za Kenya (Kenya
Professional Boxing Commission, UPBC), Uganda (Uganda Professional
Boxing Commission, UPBC na Tanzania Professional Boxing Commission, TPBC
zilikutana mjini Moshi na kuunda rasmi Shirikisho la Ngumi za Kulipwa
la Afrika Mashariki na Kati (East & Central Africa Professional
Boxing Federation au ECAPBF.
Katika
mkutano huo uliohudhuriwa na Marais wa Kamisheni hizo tatu Celestino
Mindra (UPBC) Memba Muriuki (KPBC) na Onesmo Ngowi (TPBC) uliweka
uongozi wa Shirikisho la ECAPBF kama ifuatavyo:
No comments:
Post a Comment