Estadio Santiago Bernabéu - Madrid 18/09/2012 - 20:45CET (20:45 local time)
| 3-2 |
Cristiano Ronaldo akishangilia bao la tatu aliloifungia Timu yake katika ushindi wa tatu kwa mbili ndani ya uwanja wa santiago Bernabau uispania
Bao la Cristiano Ronaldo katika dakika ya mwisho ya
mchezo liliiwezesha klabu ya Real Madrid kuishinda Manchester City
magoli 3-2 walipowakaribisha katika uwanja wao wa Bernabeu nchini
Uhispania, mechi ya klabu bingwa barani Ulaya.
Kipa Joe Hart kwa muda mrefu aliiwezesha Man
City kuendelea vyema pasipo kufungana mabao katika mechi ya Jumanne
usiku, hadi Edin Dzeko alipowashangaza wenyeji kwa kupata bao katika
kipindi cha pili.
Marcelo
alisawazisha, kupitia mpira ambao ulimgusa mchezaji wa City kabla ya
kubadilisha mwendo, lakini City wakafanikiwa kuendelea tena kuongoza
baada ya mkwaju wa free-kick kutoka kwa Aleksandar Kolarov, wakati mpira moja kwa moja ulielekea hadi wavuni.
Kisha Karim Benzema aliweza kusawazisha, kabla ya Ronaldo kuandikisha bao la tatu na la ushindi katika mechi hiyo, na matokeo yakawa 3-2.
Kisha Karim Benzema aliweza kusawazisha, kabla ya Ronaldo kuandikisha bao la tatu na la ushindi katika mechi hiyo, na matokeo yakawa 3-2.
Kati ya mechi nyingine za klabu bingwa barani
Ulaya ilikuwa ni pamoja na mchezo wa Arsenal, ambayo ilianza kampeni
yake ya 15 ya mashindano hayo kwa kuwashinda wageni katika michuano
hiyo, Montpellier ya Ufaransa.
Timu ya Arsene Wenger ililemewa ugenini baada ya
dakika tisa, wakati nahodha Thomas Vermaelen aliposababisha
penalti,ambayo ilifungwa na Belhanda, lakini kutokana na magoli mawili
ya Arsenal kupatikana kwa haraka katika kipindi cha kwanza, kutoka kwa
Lukas Podolski na Gervinho, hali ya mchezo ilibadilika, na Arsenal
ikapata ushindi wa magoli 2-1.
Ushindi huo unamaanisha Arsenal na Schalke ya Ujerumani ndio vilabu ambavyo vinaongoza katika kundi B.
No comments:
Post a Comment