Mwishoni wa juma hili Cape Verde na Ethiopia zilidhihilisha ya kuwa David Bado ameshindwa kupigana na Goliath kwa wale wanaojua Biblia wanajua hadithi hiyo Baada ya mataifa makubwa katika soka ya afrika kutupwa nje katika kuwania Tikiti za kucheza mashindano ya mataifa ya afrika yatakayo fanyika afrika kusini huku 2013 kuku mchezo wa fainali ukichezwa katika uwanja Soccer City Katika jiji la Johannesburg.
Cameroon imeshindwa kufuzu kwa mara ya pili mfululizo katika michuano hii baada ya kuchemka kuifunga Timu ya taifa ya Cape Verde 3-2 katika sheria ya magoli ya nyumbani na ugenini ambapo nchi ya cape Vede ina watu laki tano 500,000 tu.
Camroun waliingia kiwanjani wakiwa nyuma kwa magoli 2-0 waliyofungwa wiki iliyopita huko praia, simba hao wanyika walishtushwa tena katika kiwanja chao cha nyumbani baaada ya Heldon Nhuck kuipa Cape Verde Goli la kuongoza 1-0 Dhidi ya Wenyeji Cameroon katika mji mkuu wa nchi hiyo Yaounde.
katika mashindano hayo yatakayoanza january mwakani huko afrika kusini timua yaifa ya Ethiopia, ambayo imeifunga sudan nayo itakuwemo katika mshindano baada ya miaka Thelathini baada ya kutoka na ushindi wa mabao matano kwa matatu
michuano ambayo itachezwa mwakanai imerebishwa kiratiba ambapo ilikuwa ikileta mzozo dhidi ya michuano mikubwa ya dunia na ulaya sasa itakuwa ikichezwa katika mwaka usio gawanyika kwa mbili ilikuondoa msuguano huo
Timu ya mwisho kutinga katika mashindano hayo ni Angola mara baada ya kuifumua zimbabwe mabao matatu kwa moja katika mchezo wa kwanza mchezaji wa Zamani wa Manchester united Manucho alifunga mabao mawili ya kichwa ndani ya dakika nane za kipindi cha kwanza na kuipatia ushindi timu yake ya Angola ushindi malidadi.
No comments:
Post a Comment