Mabingwa wa kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati
almaarufu kombe la Kagame, timu ya Young Africans Sports Club imeifunga
timu ya Black Leopard ya Afrika Kusini mabao 3-2 katika mchezo wa
kirafiki uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaaam.
Young Africans iliyokuwa nje ya nchi kwa kambi ya
mafunzo takribani wiki ilikuwa ikicheza mbele ya washabiki wake, iliweza
kucheza soka safi na la kuvutia kipindi chote cha mchezo huku Black
Leopard ikipata wakati mgumu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Didider
Kavumbagu alikosa bao la wazi dakika ya 21 ya mchezo akiwa yeye na
mlinda mlango wa Black Leopard Ayanda Mtshali, lakini shuti alilopiga
lilipaa juu ya lango la timu hiyo.
Heka heka langoni kwa Yanga kama anavyo onekana mlinda Mlango wa Yanga Said
Mohamed akijaribu kuokoa hatari hiyo langoni kwake.
Wana Yanga kutoka
Pugu Kigogo Fresh wao walikodi daladala kwenda kuona mchezo
huo.
Yanga
iliednelea kuutawala mchezo kwa wachezaji wake kupigiana migongeo mizuri
na kuutawala mchezo hasa eneo la kiungo, Kabange Twite alishindwa pi
akuipatia Yanga bao katika dakika ya 25 baada ya kushinda kumalizia pasi
safi ya Mbuyu Twite.
Dakika ya 32 Jerson Tegete
aliipatia Young Africans bao la kwanza kwa mkwaju wa penati kufuatia
mlinzi wa Balck Leopard Harry Nyirenda kumuangusha Haruna Niyonzima
katika eneo la hatari, amabpo mwamuzi Hashim aliamuru upigwe mkwaju wa
penati na Jerson Tegete kuukwamisha mpira huo wavuni.
Yanga
iliongeza kasi ya kusaka bao la pili lakini shambulizi liliofanywa na
Mbuyu Twite liliokolewa na mlinda mlango wa Black Leopard Matshal kabla
ya Mbuyu tena kupiga kichwa kilichopaa mita chahce juu ya lango la timu
ya Black Leopard.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Young Africans 1 - 0 Black Leopard.
Frank Domayo wa Yanga
(chini) akimshika jezi Mlinzi wa Black Leopards, Humahrey
Khoza.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo kocha
Brandts aliwatoa Kabange Twite, Mbuyu Twite na golikipa Ally Mustafa
'Barthez' nafasi zao zikachukuliwa na Juma Abdul, Saimon Msuva na
golikipa Said Mohamed.
Dakika ya 47, Humphrey
Khoza aliipatia Black Leopard bao la kusawazisha kwa kichwa akiunganisha
mpira wa kona uliopigwa na Edagr Manaka kufutia kutokuwepo kwa
mawasilaino kati ya mlinzi Nadir Haroub na mkinda mlango wake Said
Mohamed.
Kiungo chipukizi Frank Domayo aliipatia
Young Africans bao la pili dakika ya 63 ya mchezo, akimaliza pasi safi
iliyopigwa na kiungo Haruna Niyonzima na mpira huo kumkuta Domayo ambaye
alimchambua mlinda mlango wa Black Leopard Mtishal na kuhesabu bao la
pili.
Dakika 10 baadaye mshambuliaji Jerson Tegete
aliipatia Young Africans bao la tatu kwa umakini akimalizia pasi ya
kungo mshambuliaji Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa timu ya Black
Leopard na kumpasia mfungaji aliyeukwamisha mpira huo wavuni.
Jerson
Tegete nusra angeipatia Young Africans bao la nne, kufuatia lakini
krosi iliyopigwa na Saimon Msuva kuokolewa na mlinzi wa Black Leopard
sentimeta chache pemebeni mwa lango huku Tegete tayari akiwa tayari kwa
kuukwamisha mpira huo.
Dakika ya 89, Black Leopard
ilijipatia bao la pili kwa mkwaju wa penati kupitia kwa mshambuliaji
wake Rodney Magalela kufuatia mlinzi wa kulia wa Young Africans kumcheza
madhambi mshambuliaji huyo katika eneo la hatari.
Mpaka mpira unamalizika Young Africans 3- 2 Black Leopard.
Kocha
mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake kwa kupata
ushindi huo wa leo, kwani timu ya Black Leopard ni timu nzuri, imecheza
vizuri lakini mwisho wa siku vijana wangu walikuwa ni bora zaidi ndio
maana wameibuk ana ushindi huo.
Kambi yetu ya
mafunzo nchini Uturuki imetusaidia sana, wachezaji wanacheza kwa
kujiamini wametulia hawana presha ya mchezo, hali inayopelekea kucheza
migongeano kwa uhakika na hii ni dalili tosha kuwa tupo tayari kwa
mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom alisema 'Brandts'
Young Africans:
1.Ally Mustapha 'Barthez'/Said Mohamed, 2.Mbuyu Twite/Juma Abdul,
3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman
Idd 'Chuji', 7.Kabange Twite/Saimon Msuva, 8.Frank Domayo, 9.Didier
Kavumbagu/Said Bahanuzi, 10.Jerson Tegete/George, 11.Haruna Niyonzima
Black Leopard:
1.Ayanda Mtshali, 2.Ernort Dzaga, 3.Nkosiyabo Xakane, 4.Harry Nyirenda,
5.Humphrey Khosa, 6.Munganga Djunga Jean, 7.Mongezi Bobe, 8.Thomas
Madimba, 9.Abbas Amidm, 10.Edagr Manaka 11.Rodney Ramagalela
No comments:
Post a Comment