KOCHA wa timu ya taifa
ya Nigeria, Steven Keshi ataendelea kuifundisha timu hiyo baada ya
waziri wa michezo wa nchi hiyo Bolani Abdullahi kufanya mazungumzo ya
kina na kocha huyo. Mgogoro
uliopo kati ya Keshi na Shirikisho la Soka la Nigeria-NFF lilipelekea
kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 kutangaza kujiuzulu katika kituo cha
redio cha Metro FM nchini Afrika Kusini.
Lakini
mara baada ya waziri huyo kufanya naye mazungumzo jana jijini
Johannesburg alifanikiwa kumshawishi kocha huyo kuendelea na kibarua
chake ingawa haikufafanuliwa kwa undani mazungumzo yao yalihusiana na
nini. Pia kuna
taarifa kuwa mazungumzo ya usuluhishi kati ya Keshi na NFF yataendelea
wakati timu hiyo itakapowasili jijini Abuja baadae leo.
No comments:
Post a Comment