Kenya Imepata tikiti ya kuandaa mashindano ya kombe la chalenji Shirikisho la soka la kenya (FKF) limepata haki hiyo katika mkutano wa CAF uliofanyika huko
Marrakech, Morocco.
Ambapo Mechi zitachewza katika kiwanja cha kimataifa cha Moi na Nyayo huko Nairobi pamoja na
Kisumu Uwanja wa Moi ambao kwa sasa upo kweneye matengenezo ambao unafadhiliwa katika mradi wa fifa ( FIFA Goal
Project) utakuwa tayari baada ya miezi mitatu .
"Huu ni wakati mzuri kwetu kwa soka la kenya na tunashukuru kwa msaada wa serikali na tunaamini tutaandaa mashindano bora zaidi katika ardhi ya kenya alisema Mwenyekiti wa shirikisho la soka la kenya ," FKF Sam Nyamweya .
"Vile vile tumeomba kuaanda michuano ya vilabu bingwa afrika mashariki na kati na kutakuwa na mkutano wa cecafa kuatazama uwezekano wa jambo hilo .
Kenya iliandaa mara ya mwisho michuano hiyo mwaka 2009 na mwaka jana ilishindwa kuaandaa mashindano na uganda .
No comments:
Post a Comment