Mzee Joseph Itangile maarufu kama mzee Kinesi akitangaza mabadiliko ya uongozi wa juu wa klabu ya Simba ikiwa ni siku moja tu baada ya Zakharia Hans Poppe na Geofrey Nyange Kaburu kubwaba Manyanga. |
Kaimu mwenyekiti mpya wa kamati ya usajili na ushindi ya Simba. |
Baada
ya siku moja kupita kufuatia viongozi wawili wa kamati ya utendaji ya
Simba kutangaza kujiuzulu, mwenyekiti wa baraza la wadhamini la klabu ya
Simba mzee Joseph Itangile maarufu kama mzee Kinesi hii leo ametangaza
mabadiliko ya dharura ya uongozi wa klabu ya klabu hiyo.
Katika
mabadiliko hayo mzee Kinesi amesema kuanzia hii leo nafasi iliyokuwa
ikishikiliwa na Hans Poppe aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya
klabu hiyo sasa itakuwa ikishikiliwa na Bi Rahma Al Harouz( malkia wa
nyuki) huku nafasi ya makamu mwenyekiti wa klabu hiyo iliyokuwa
ikishikiliwa na Geoffrey Nyange Kaburu sasa itakuwa ikikaimiwa na yeye
mwenyewe.
Mabadiko
hayo yamefuatia kikao cha dharura cha wajumbe wa kamati ya utendaji ya
Simba kilicho fanyika jana usiku bila ya kuwepo mwenyekiti Alhaji Ismail
Aden Rage ambaye yuko nchini India akifanyiwa matibabu ambaye hata
hivyo baada ya mawasiliano kufanyika alikubali na kubariki mabadiliko
hayo.
Mzee
Kinesi amesema kwamba kwasasa klabu ya Simba bado ina umoja na katika
kipindi hiki wameunda kamati ya ushindi ambayo itakuwa chini ya Malkia
wa nyuki na kwamba ni wakati wa kuondoa mipasuko ndani ya klabu hiyo.
Jioni
hii uongozi wa klabu ya Simba umetembelea tawi la mpira pesa kwa lengo
la kuvunja mpasuko ndani ya klabu hiyo na kujenga umoja.
No comments:
Post a Comment