Timu ya soka ya azam fc imejihakikishia nafasi ya pili baada ya kuifunga Mgambo jkt katika mechi ya ligi ya vodacom Tanzania Bara kwa kuibamizaa mabao matatu kwa bila mabao ya azam yamefungwa na John Bocco Adebayor ,Jorkings Artudo ,aidha Kipre Tchetche amefunga bao lake la kumi na saba katika ligi hiyo ya Vodacom kwa maana hiyo Azam fc inafaikisha Alama 51 katika nafasi ya pili huku Yanga ambao ni mabingwa wa ligi ya Tanzania Bara wakiwa wana alama 57 baada ya michezo ishirini na Tano huku simba ikiwa katika nafasi ya tatu na alama 45 ambapo hata kama watawafunga wapinzani wao Yanga jumamosi ijayo wataendelea kusalia nafasi ya tatu na hawata pata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa na kuziacha Azam fc Na Yanga kushiriki mashindano ya kimataifa huku yanga wao wakiwa wanashiriki klabu afrika na Azam fc wakiwa wanashirki mashindano ya Kombe la shirikisho barani afrika .
No comments:
Post a Comment