HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

26 October 2012

Wanyama kuihama Celtic


Mcheza kiungo wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee stars, anayeichezea klabu ya Celtic ya Scotland Victor Wanyama, anaripotiwa kudinda kusaini kandarasi mpya na klabu hiyo ya Celtic.
Kandarasi ya wanyama na klabu hiyo ya Celtic inatarajiwa kukamilika mwaka wa 2015, na klabu hiyo ilikuwa na matarajio ya kuumpa mchezaji huyo kandarasi mpya, ili kuzuia uwezekano wa mchezaji huyo kuhamia vilabu vingine, vinavyoshiriki kwenye ligi kuu ya Premier ya England ambavyo vimeonyesha nia ya kumsajili kama vile Manchester United.
Lakini Wanyama mwenye umri wa miaka 21 na ambaye alijiunga na Celtic kutoka kwa klabu ya Beerschot ya Ubelgiji mwaka wa 2011, haamini kuwa kandarasi hiyo mpya inawiana na dhamani yake kwa sasa na hivyo amekataa kuisaini.
Kwa mujibu wa agenti wa Wanyama, Rob Moore, tayari Celtic imefahamishwa kuwa kandarasi hiyo haikithi matarajio ya mchezaji huyo.
Ripoti zinasema klabu hiyo ya celtic ilikataa ombi kutoka kwa vilabu kadha ambavyo vilikuwa vikitaka kumsajili mchezaji huyo mapema mwaka huu.Kuna fununu kuwa huenda mchezaji huyo akahamia England msimu ujao wa usajili na miongoni mwa vilabu ambavyo vimeonyesha nia ya kumsajili ni pamoja na Manchester United,Manchester City na Tottenham.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers