Colombia itapambana na Brazil katika Robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 Baada ya Kuibamiza Mabao mawili kwa sifuri yalyofungwa na James Rodriguez na kuipatia Ushindi Dhidi Uruguay.
Rodriguez, 22, alifunga la kwanza kwa ufundi wa aina yake baada ya kugeuka na mpira hewani kutoka Takriba Mita 20 au Yard 25 ambapo mpira huo uligonga chini ya Besera na kutinga wavuni.
Uruguay, ikicheza bila Luis Suarez aliyefungiwa miezi minne,walikuwa wadhaifu na muda mwingi wa Mchezo walikuwa wakilinda zaidi Goli hasa katika Nusu ya Kwanza ya Mchezo .
Rodriguez alifunga tena kwa shuti kali na kufunga goli lake la Tano katika mashindano ya Kombe la Dunia.
Uruguay walimailiza kipindi cha pili kwa nguvu kubwa lakini walishindwa kupunguza angalau Goli moja, Maxi Pereira's alijaribu kufanya kama alivyofanya Rodriguez lakini mpira uliishia mikononi mwa mlinda Mlango David Ospina ambaye baadaye alidaka mpira uliopigwa na Edinson Cavani.
No comments:
Post a Comment