Klaas Jan Huntelaar amefunga kwa mkwaju wa penati ulio wasukuma nje ya timu ya soka ya Taifa ya Mexivo katika dakika za lala salama na kuipatia ushindi mzuri timu ya taifa ya uholanzi ambayo inakuwa timu ya tatu kuingia Robo fainali .
Waholanzi ndio walikuwa nyuma kwa Goli moja katika kipindi chote cha pili cha mchezo lakini zikiwa zimesaria dakika chache mpira kwisha Wesley Sneijder aliachia shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa wa Mexico ,Ochoa .
Lakini dakika mbili baadae kabla mpira kumalizikaArjen Robben
aliofanyiwa faulo na Rafael Marquez, na kumuachia Mchezaji aliyetokea kwenye benchi Huntelaar kufunga Goli la Ushindi .
Giovani dos Santos ndiye aliyeipatia Mexico Goli la kuongoza mara baada ya kupiga shuti la Yard 25-.
Louis van Gaal's na timu yake sasa watapambana na Costa Rica au Greece katika robo fainali .
Aidha mechi hii kulishuhudiwa kwa mara kwanza wachezaji wakipata mapumziko ya Dakika Nne kupata maji kutokana na Joto kali linaloendelea Nchini Brazil
No comments:
Post a Comment