Costa Rica sasa itapambana na Netherlands katika Robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuwaondoa Ugiriki kwa Mikwaju ya Penati .
Mechi ilikwisha katika Dakika mia moja na Ishirini kwa timu hizo kutoshana Nguvu ya Goli moja moja baada Sokratis Papastathopoulos's kusawazisha Goli katika Dakika ya za Majeruhi na kuisawazishia Ugiriki .
Bryan Ruiz Ndiye aliyepatia Costa Rica Goli la kuongoza hiyo ilikuwa Kabla ya mchezaji mwenzake Oscar Duarte kulimwa kadi ya Pili ya Manjano na kutolewa Nje kwa Kadi Nyekundu .
Dakia thelathini za Nyongeza zilishinwa kutoa Mshindi na katika mapigo ya Penati Theofanis Gekas alikosa , na Kuumpa nafasi Michael Umana kuipatia Costa Rica ushindi sasa watapambana na Uholanzi katika hatua ya Robo fainali.
No comments:
Post a Comment