Timu ya soka ya Taifa ya Nigeria imekuwa timu ya kwanza kufuzu katika hatua ya kumi na sita Bora kutoka Afrika licha ya kufungwa mabao matatu kwa mawili na Argentina katika michuano ya kombe la Dunia inayoendelea Nchini Brazil katika mchezo wa Kundi F uliochezwa katika uwanja wa Estadio Beira-Rio (Jose Pinheiro Borda) .
Argentina ndio waliokuwa wa kwanza kupata Goli katika dakika ya Tatu likifungwa na Mesi na dakika ya nne Ahmed Musa kusawazisha lakini Lionel mesi alifunga Goli la pili dakika moja kabla ya Mapumziko lakini kipindi cha pili Ahmed Musa tena aliisawazishia Nigeria goli la pili lakini Tafrija hiyo haikudumu sana Kwani Marcos Rojo alifunga bao la tatu katika Dakika ya Hamsini .
Matumaini ya timu ya soka ya taifa ya iran kufuzu hatua ya pili ya kumi na sita Bora kwenye michuano ya kombe la Dunia yameishia hewani baada ya kufungwa na timu ya taifa ya Bosnia-Hercegovina licha ya timu hiyo kutolewa .
Timu hiyo inayoongozwa na kijana wa Kimakonde Carlos Queiroz's wangeweza kufuzu katika hatua ya pili lakini uchache wa alama kibindoni ndio uliowagharimu Edin Dzeko aliipatia Bosnians goli la kuongoza kwa shuti la mita 25 yards.
Roma's Miralem Pjanic alifunga goli la pili katika kipindi cha pili
Reza Ghoochannejad alisawazishia goli moja lakini Avdija Vrsajevic alifunga bao la tatu na kuipatia Bosnia Ushindi wa kwanza katika kombe la Dunia
1 | Argentina | 3 | 3 | 9 | |||
2 | Nigeria | 3 | 0 | 4 | |||
3 | Bos-Herce | 3 | 0 | 3 | |||
4 | Iran | 3 | -3 | 1 |
No comments:
Post a Comment