Tim Krul amekuwa shujaa wa uholanzi akitokea kwenye Benchi na kucheza kwa dakika moja tu baada ya kuingia kwa kazi ya kucheza penati na ameokoa penati na kuisaidia Netherlands kuifunga Costa Rica kwa mikwaju ya penati na sasa watakwaana na Argentina.
Krul aliokoa penati zilizopigwa na Bryan Ruiz na Michael Umana na kuivusha Uholanzi .
Mchezo huo ulimalizka kwa kutokufungana kati ya timu hizo katika dakika mia moja na ishirini , Huku Wesley
Sneijder akigongesha Nguzo za Goli mara Mbili wakati Robin van Persie jitihada zake za kutafuta Goli zikiishia kwenye kugongesha Nguzo za Goli .
Uholanzi sasa wanakutana na Argentina kwenye nusu fainali ,ambao waliwafunga wa belgiji katika mechi ya mwanzo . .
No comments:
Post a Comment