Naam nachukua fursa kuwapongeza watu waliofanya kazi ya kuwaleta Real Madrid lakini pili naenda moja kwa moja kwenye hoja ya Msingi Hivi waandishi wa Habari za Michezo tunakosa gani pale uwanja mpya wa Taifa ?
Kwa mashabiki, kuna Eneo moja ambalo ninyi Halimjui linaitwa Mixed zone hii ni sehemu ambayo waandishi wanahaki ya Kuzungumza na wachezaji kufanya nao mahojiano tena kistaarabu kabisa na Kama unavyojua waandishi wa Habari wote wanavitambulisho maalum na wengi wao wanakamera zao Tape na Digital recoder yaani vinasia sauti .
Mara kadhaa zinapokuja timu kubwa zenye mastaa Ndipo hari inapozidi kuwa mbaya Hakuna mwandishi wa Habari anayekuja na Kisu uwanjani wala Bakora au Bunduki lakini mtu unasukumwa kanakwamba unakwenda kumdhuru mchezaji Hivi hii ni haki ?
Walinzi waliopo kwenye uwanja wa Taifa tunajua kabisa wapo kazini lakini kazi yake ni kunilinda mimi na mchezaji pia kwenye Eneo la Mixed zone hakuna raia wa kawaida anayeweza kuingia Bila kitambulisho .
lakini Bado unabanwa hasa wanapokuja mastaa wa Kidunia kama waliokuja wiki hii Figo ,karembeu,na Canavaro
Kifupi ni kwamba kabla ya watu hawa kuja wanahabari walioneka msaada mkubwa lakini baada ya mechi kumalizika tulionekana kama Genge la Wahuni lakini hii ni kwasababu kubwa kazi tuliyopfanya ilishakwisha aisifie mvua imemcheshea hawa walinzi wanatakiwa kueleweshwa tu jinsi ya kukaa na sisi kwa sababu hatuna uwezo kwa kupambana nao kiuweredi wa kinguvu hatuwezi.
Mtu anayezuia mwandishi wa habari kuongea na wachezaji tumueleweje ?
Mpenzi msomaji wangu hii ni hatari sana kitendo cha kuwanyenyekea mastaa hawa kama mitume ya Mbiguni sio haki kabisa hawa mastaa wanakuja mara moja kwa mwaka sisi tunabaki hapa kuna haja gani ya kutunishiana misuli uwekwe utaratibu tu wa jinsi ya kuelewana nao kwa sababu bila hivyo waandishi wa habari tutaonekana kama wahuni tu.
Naomba niishie hapa kwasababu hasira zinanipanda naogopa kutukana .
No comments:
Post a Comment