HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

17 April 2009

WAKUCHUNGUZWA NI PINDA NA SIYO DECI!

Mwenyekiti wa cha Democratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila amesema kuwa Waziri mkuu Mizengo panda ndiye anayetakiwa kuchunguzwa na siyo DECI Mtikila ambaye amesema kuwa wataitetea DECI kwakuwa ndio itikadi ya chama chao na wanajua ni jinsi gani DECI ilivyowakomboa walalahoi walikuwa wamekata tamaa kimaisha “unajua kwenye hii DECI waliokopa ni wanajeshi ,polis,i magereza na watu wengine wenye vipato duni vilevile watu wanasomesha watoto wao unajua huyu waziri mkuu pinda anaipiga marufuku DECI na wanasema kuwa mabenki hayana pesa kwa sababu watu wamehamisha pesa zao wameenda kuwekaza DECI si unajua uchaguzi unakaribia sasa watakosa sehemu ya kwenda kukopa kwa ajiri ya uchaguzi” hivyo ndivyo mchungaji Christopher Mtikila anavyo fafanua . Mchungaji Christopher akaendelea kusema mimi nashangaa mnasema DECI ni wezi kuna mtu yeyote Yule ambaye amekwenda mahakamani kulalamika kuwa ameibiwa pesa zake na DECI lawama ambazo nazisikia mimi ni za watu kufaidika na DECI sasa huyu pinda vipi halafu ukiangalia ni waziri mwenye akili timamu anaongea mambo kama haya sasa ukitaka kuona hatufai kule bungeni alidiliki kusema wauwaji wa albino wauwawe katika sheria hata kama mtu kawauwa watu kiasi gani na Yule mtu bado ni safi mpaka mahakama ithibitishe kuwa ameuwa ndiyo itoe hukumu sasa wewe unaposema auwawe unamaana gani ukiwa kama waziri mkuu hilo awakumtaka waziri mkuu ajiuzulu kwani waliliona ni la kawida jamani tunakwenda wapi. Jamani hamuoni kama hizi ni fitna tuu kwani ukiangalia hii DECI inapata ushauri kutoka B.O.T na ina TIN number na inalipa kodi ya mapato ya serikali yetu inaajiri wafanyakazi rasmi na kuwa changia kwa mujibu wa sheria katika mfuko wa NSSF. SIYO SIRI! Tunajua kwamba saccos kama za akina mengi na vikoba vyake,pride ya akina iddi simba , mabaenki ya kama akiba benk ,CRDB ,NMB, Zipo katika hari mbaya kwani wateja wao wenye akili timamu wamesha hamisha pesa zao na kupeleka DECI ambako wana vuna na kupanda kinachofuta kwa DECI sasa hivi nikwenda kukata bina ya benki Israel ili endapo itatokea mtu kaiba basi iende kutoa maelezo kuwa imeibiwa kwa mtindo gani ili ipate pesa za kuwarejeshea wale ambao wanadai pesa zao Mchungaji na malizia kwa kusema kwa sababu wamekosa vipawa vya kubuni za kuishinda DECI na kulinda biashara kihalali, wanachoweza ni uharamia tu dhidi ya DECI kwani mizengo panda na chama chake cha CCM wapo katika mkakati wa wa kuleta mapesa ya walalahoi huko DECI kwa ajiri ya uchaguzi wa busanda na ule wa mwakani kwani wanakochota pesa zetu kuna waka moto. Naam hivi ndivyo mambo yalivyo nduguzanguni .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers