Mpenzi msomaji wa Kurasa hii karibu tena kwa safu yangu leo nimeona tuangazie sakata kubwa ambalo linaonekana kushtua mioyo ya watu wengi Nchini Tanzania . Kuna msemo mkubwa unaosema makocha huajiriwa ili wafukuzwe yamekuwa ni mazoea kuutumia msemo huu Sehemu Kadhaa lakini naomba tutazame kwa kina kwanini makocha wa wanaokuja Tanzania huishia kufukuzwa ?
Msimu wa mwaka 2013/14 katika timu kumi na nne ni makocha wawili tu ndio walio dumu kufundisha timu zao za ligi kuu Juma mwambusi Mbeya city na Mecky Mexime Mtibwa sukari makocha waliosalia wote walifukuzwa kwa maana walioanza sio waliomaliza ! Labda la kwanza tutazame kwanini yanatokea haya . timu ya soka ya Taifa ya Tanzania imefundishwa na makocha wakuu wanne mpaka sasa Maximo,Jpoulsen,kim poulsen,na sasa Mart Noij wakiwa na wasaidizi wao tofauti na katika kipindi chote hicho klabu za Tanzania zimekuwa zikifundishwa na makocha tofauti tofauti na kwa maana hiyo hata wachezaji wamekuwa wakifundishwa farsafa tofauti kwa mara kadhaa .
Ukitazama kwa upande wa mafanikio kwa makocha wote hao hakuna hata timu moja si klabu wa taifa Stars iliyofanikiwa katika hatua kubwa japokuwa Taifa stars iliishia kushiriki (chan) yaani mashindano ya mataifa ya afrika kwa wachezaji wa Ndani, Jambo ambalo sio la Kujivunia sana .Swali langu la msingi ni jambo gani kubwa hasa au kwanini makocha wanafukuzwa kila kukicha na wengine wakirejea kufundisha klabu walizofukuzwa mara kadhaa .tunachogundua hapa ni kuwa lazima tujiulize maswali ya msingi makocha hawajui kufundisha ? je wachezaji wetu wanaelewa? kwanini iwe makocha ndio wanaukuzwa kila siku na sio wachezaji
kwa miaka zaidi kumi hakuna hata timu hata moja ya Tanzania iliyofanya jambo la maana katika mashindano ya kimataifa na mafanikio yao makubwa yamekuwa ni kutwaa ubingwa wa Tanzania tu na wakijitahidi Ubingwa wa Cecafa je kuna shida gani na sio Tanzania hata afrika mashariki tunatatizo hilo je kuna tatizo gani?
Pengine yafuatayo yanaweza kuwa sababu uelewa Mdogo wa wachezaji husika pindi wawapo mazoezini na kusingizia mazoezi magumu kumpakazia kuwa kocha ni mkali au anatukana lakini kuna kocha asiyetukana kiwanjani ? yapo mambo mengi ambayo makocha wa kigeni wanapokuja hutaka kutuletea kwenye mstari lakini hushindikanika kwa sababu ya tabia zetu mbaya za ukaidi je unafikiri hawa makocha tunaowafukuza wanaizungumziaje Tanzania pindi wawapo makwao je mchezaji wa kitanzania anapokwenda kujaribu soka ulaya unafikiri kwanini wanashindwa kwasababu wanafanya upembuzi kukujueni tabia zenu kiukweli tutafukuza makocha mpaka mwisho wa Dunia na hatutofanikwa kamwe kushinda chochote kwa sababu ya kuwalea watoto kama yai katika soka sio Jambo rahisi hata kidogo.
Hari iliyopo sasa lazima tutawaona makocha hawajui kufundisha na tutasingizia vitu vingi sana lakini jambo la msingi ni kuu je wachezaji hawa wanafundishika na hapo ndipo utakapoona kuwa mfumo mzima wa soka la Tanzania una matatizo makubwa na haijulikani yatakwisha lini .
No comments:
Post a Comment