UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema kuwa umekiri kupokea barua kutoka kwa kitengo cha
Wanasheria (Maleta& Ndumbaro Advocate ya Dar) ikisema kuwa timu hiyo imeshindwa kumlipa Abdi Banda mshahara wa miezi mitatu mfululizo kwa kusema imevunja mkataba.
Wanasheria (Maleta& Ndumbaro Advocate ya Dar) ikisema kuwa timu hiyo imeshindwa kumlipa Abdi Banda mshahara wa miezi mitatu mfululizo kwa kusema imevunja mkataba.
Akizungumza
jana,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amekanusha kwa kusema
kuwa habari zilizoenezwa kuwa walishindwa kumlipa mshahara mchezaji huyo
sio za kweli bali kilichotokea ni kwamba banda alifundishwa na watu
wajinga kwamba asichukue mishahara yake ya miezi
mitatu ili kukipa hadhi kipengele hicho cha sheria kilichopo kwenye mkataba wake,
“Akinukuu kipengele cha ibara ya
3(3.2)(1) cha mkataba wa Banda kinachosema kuwa ikiwa klabu imeshindwa
kumlipa mchezaji mishahara yake ya miezi mitatu mfululizo basi mkataba
wa mchezaji huyo na klabu umevunjika “Alisema El Siagi.
Alisema lakini alichokifanya mchezaji
Banda ni kukwepa kuchukua mishahara yake makusudi ili ionekane kwamba
hakulipwa miezi mitatu .
El Siagi alisema alichokifanya ni mambo
mawili, jambo la kwanza ni kudanganya wanamichezo hapa nchini na klabu
yake ya Coastal Union ili aipatie fedha Klabu ya Simba ambao huo ni Wizi
wa kutumia hila.
Alisema la pili ni kitendo cha kusaini
mkataba Simba wakati akijua ana mkataba na Coastal Union ambao
unatarajiwa kuishia Juni 2016.
Katibu huyo alisema ni makosa makubwa
mchezaji huyo kusaini mikataba miwili tofauti katika kipindi cha msimu
mmoja kwa sababu atakuwa amevunja taratibu za mikataba kutokana na kuwa
mchezaji hawezi kuwa na mikataba miwili kwa wakati mmoja.
Aidha alisema kutokana na mchezaji huyo
kudanganya na kukiuka utaratibu wa mkataba, Uongozi wa Coastal Union
umejipanga kumchukulia hatua kali mchezaji huyo ikiwemo hatua za
kinidhamu.
Katibu huyo alisema anashangazwa kuona
kuwa klabu ya Simba yenye viongozi wazoefu kwenye masuala ya mpira
wanafanya makosa kama hayo kwa kutokufuata taratibu za kiusajili.
“Kanuni za shirikisho la soka Dunia
(FIFA) na Shirikisho la soka nchini (TFF) zinasema mchezaji hawezi
kuzungumza na timu yoyote wakati akiwa ndani ya mkataba mpaka labda awe
amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake ndio anaruhusiwa kuzungumza na
uongozi wa klabu nyengine.
Aliongeza kuwa iwapo mchezaji akiwa
amebakiza mwaka mmoja basi klabu na klabu ndio zinaruhusiwa kuongea na
sio mchezaji hivyo Banda bado ana miaka miwili Coastal Union ambayo
imebaki hivyo Simba walichotakiwa kufanya ni kuzungumza na uongozi wa
Coastal union ili
kumnunua mkataba wake badala ya kurubuniwa na kauli hafifu za kiudanyanyifu.
Katibu huyo alisema kwa kufanya hivyo
Coastal Union kupitia wanasheria wake ,Divine Chambers Advocates &
Hamidu Mbwezeleni wanajipanga kuwaandikia barua shirikisho la soka
nchini (TFF) pamoja na Simba ili
kudai fidia ya Ukweukwaji wa taratibu hizo.
Alieleza kuwa tayari Coastal Union
wamemtumia mwanasheria wa Banda majibu ya barua yake kupitia mwanasheria
Divine Chambers Advocates ya Mjini Tanga
No comments:
Post a Comment