HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

7 November 2014

JE RUVU SHOOTING ITAWEZA KUTOA SULUHU KWA SIMBA



Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii ambapo tiketi za elektroniki hazitauzwa tena kwenye magari, hivyo washabiki wanunue tiketi hizo kwenye mtandao au kwenye maduka ya CRDB Fahari Huduma.

Kesho (Novemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutakuwa na mechi kati ya Yanga na Mgambo Shooting wakati Uwanja wa Chamazi kutakuwa na mechi kati ya Azam na Coastal Union. Jumapili ni mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting.

Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Taifa ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 (VIP B na C) wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Mechi za Uwanja wa Chamazi kiingilio ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000.

Mechi nyingine za VPL kesho ni kati ya Stand United na Mbeya City (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Mtibwa Sugar na Kagera Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo ya saba itakamilika Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Ndanda kutoka Mtwara.

Wakati huo huo, mchezaji bora wa VPL kwa mwezi Oktoba, Salum Abubakar wa Azam atakabidhiwa zawadi yake kesho (Novemba 8 mwaka huu) kabla ya mechi kati ya Azam na Coastal Union

5 November 2014

VIJANA 24 KUWAVAA Swaziland


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini Mbabane.

Akizungumza Dar es Salaam, leo (Novemba 5 mwaka huu), Nooij alisema kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 10 mwaka huu saa 6 mchana kwenye hoteli ya Accomondia, na siku hiyo hiyo jioni kitafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.

Novemba 11 mwaka huu, Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwenda Afrika Kusini ambapo itaweka kambi ya siku mbili kabla ya kuondoka Novemba 13 mwaka huu kwenda Swaziland.

Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua (Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).

Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).

30 October 2014

TFF YAOMBA WADAU WABUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linakaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini. Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.

*       

Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).



Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio na Garden Avenue. Mwisho wa kupokea designs ni Novemba 15, 2014.



Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.



SDL KUANZA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 22

Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 zitakazocheza katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini itaanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu.



Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyoketi jijini Dar es Salaam jana (Oktoba 29 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange ilipitia maandalizi maandalizi ya ligi hiyo ikiwemo mwongozo wake (roadmap).



Kwa mujibu wa mwongozo huo, usajili wa wachezaji utamalizika Oktoba 31 mwaka huu. Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Novemba 1 hadi 7 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajia kukutana Novemba 11 mwaka huu kwa ajili ya kupitisha usajili.



Pia Kamati ya Mashindano imepitisha viwanja vya timu zote, isipokuwa uwanja wa timu ya Mpanda United ya Katavi na ule wa Town Small Boys ya Tunduru mkoani Ruvuma.



Uwanja wa Town Small Boys haukupitishwa kwa vile hauna uzio wa kudumu ( wa chuma) wa kutenganisha wachezaji na washabiki, na pia ufikaji wa timu Tunduru ni mgumu kutokana na ubovu wa barabara ikizingatiwa kuwa ligi hiyo itachezwa hadi kipindi cha Masika.



Kwa upande wa uwanja wa Mpanda United, umekataliwa kwa vile hauna vigezo vya msingi vinavyotakiwa ikiwemo vyumba vya kubadilishia nguo, kutokuwa na nyasi na uzio wa kudumu kutenganisha wachezaji na washabiki.



Kutokana na uamuzi huo, Mpanda United sasa itatumia Uwanja wa Mandela uliopo Sumbawanga wakati Town Small Boys itachezea mechi zake kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

29 WAITWA KIKOSI CHA MABORESHO TAIFA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia kuendelea na awamu ya pili ya maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars) inayojumuisha vijana wenye umri chini ya miaka miaka 23.

Katika awamu hii, Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ameteua majina ya wachezaji 29 ambao watakuwa wakiingia kambini mara moja kwa mwezi siku ya Jumapili baada ya kuwakilisha timu zao kwenye mechi za ligi.

Kikosi hicho cha maboresho kitakuwa kikifanya programu maalumu za mazoezi mpaka siku ya Jumatano na kucheza mechi za kirafiki na timu za ndani au nje ya nchi.

Lengo hasa la programu hiyo ni kuwajengea uwezo vijana wenye vipaji ambao walipatikana katika awamu ya kwanza ya mpango wa maboresho mwanzoni mwa mwaka huu Tukuyu mkoani Mbeya, lakini wamekuwa hawatumiki. Pia kuwandaa vijana ili kujenga timu ya ushindani na imara ya Taifa ya muda mrefu.

TFF ina imani kubwa kuwa programu hii itakuwa na manufaa kwa soka ya Tanzania. Timu hiyo itaingia kambini kwa mara ya kwanza Desemba 9 mwaka huu katika hoteli itakayotangazwa baadaye.

Wachezaji walioteuliwa ni Aishi manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Aboubakar Ally (Coastal Union), Miraji Adam (Simba), Andrew Vicent (Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel Semwanda (African Lyon) na Joram Mgeveke (Simba).

Edward Charles (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kassim Simbaulanga (African Lyon), Pato Ngonyani (Yanga), Adam Salamba (Kahama), Hassan Banda (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hashim Magoma (Stand United), Makarani Ally (Mtibwa Sugar), Said Juma (Yanga) na Said Hamis (Simba).

Aboubakary Ally Mohamed (Zanzibar), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Malombe (Geita Gold), Muzamir Ally (Mtibwa Sugar), Shiza Ramadhan (Mtibwa Sugar), Omari Nyenje (Ndanda SC), Kelvin Friday (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Alfred Masumbakenda (Kahama) na Simon Msuva (Yanga).

RAIS MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA SATA, MEYIWA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za rambirambi vyama vya mpira wa miguu vya Zambia (FAZ) na Afrika Kusini (SAFA) kutokana na vifo vya Rais Michael Sata na kipa wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa.

Ametuma salamu hizo kwa Rais wa FAZ, Kalusha Bwalya na Rais wa SAFA, Danny Jordan na kuongeza kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya ghafla vya Rais Sata na kipa huyo wa Bafana Bafana vilivyotokea wiki hii.

Rais Malinzi amesema kuwa misiba hiyo si pigo kwa Zambia na Afrika Kusini pekee bali Afrika kwa ujumla kwa vile walikuwa na mchango mkubwa kwa ustawi wa mchezo wa mpira wa miguu.

Amewaomba Rais Jordan na Rais Bwalya kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sata, na familia ya Meyiwa, na kuzitaka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo mizito kwao.


Rais Sata (77) alifariki dunia juzi kwenye Hospitali ya King Edward VII nchini Uingereza alipkuwa kwenye matibabu, wakati kipa Meyiwa aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili mjini Vosloorus.

25 October 2014

WEST HAM 2-CITY 1

 

Matumaini ya Manchester City's kutetea ubingwa  yanapata mashaka baada ya mkasa mkubwa kutoka kwa klabu ya Diafra Sakho ambaye anafunga goli kattika mechi ya sita na kuisaidia  West Ham kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja Dhidi City  .
City, wapo alama tano nyuma ya Viongozi wa ligi Chelsea, Morgan Amalfitano alimpatia pasi   Enner Valencia's ambaye alifunga goli kutoka mita tatu . 

City waligongesha mwamba mara mbili baada ya  Sergio Aguero na  Yaya Toure  kugongesha miamba hiyo Kabla ya  Sakho kuunganisha mpira wa Krosi kutoka kwa Aaron Cresswell's.
David Silva alisawazisha goli moja  baada kupigwa kona


23 October 2014

RAIS WA TOC KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA

 
Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid kesho (Oktoba 24 mwaka huu) atafunga kozi ya makocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Hafla ya ufungaji kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na kuandaliwa na TOC kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika saa 5 asubuhi kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kozi hiyo ya wiki mbili iliyoanza Oktoba 12 mwaka huu iliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Ulric Mathiot kutoka Shelisheli.

Makocha walioshiriki kozi hiyo ni Ahmed Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi), Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe (Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga), Bakari Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki Abeid (Geita).

Wengine ni Edna Lema (Morogoro), George Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo (Kigoma), Hawa Bajangero (TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said (TAFCA), Kenny Mwaisabula (TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil (Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).

Pia wapo Mohamed Ismail Laiser (Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina (Mtwara), Nicholas Kiondo (Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel Palangyo (TWFA), Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yusuf Macho (Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa).

Makocha watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za CAF wakati watakaoshindwa watapewa vyeti vya ushiriki tu.  

21 September 2014

LECEISTER YALIMALIZA SHETANI MCHANA KWEUPE

Esteban CambiassoLeicester City ilipigana kutoka nyuma ya Mabao matatu  3-1 na kujipatia ushinmdi wa bao tano kwa tatu Dhidi ya  Manchester United.
 
United walionekana washashinda mchezo pale Robin van Persie alipofunga goli  kwa kichwa na  Angel Di Maria alipochop mpira na kuifanya manchester united iongoze katika mchezo huo .
Leonardo Ulloa's alifunga goli kwa kichwa kupunguza idadi ya magoli lakini goli la kisigino la  Ander Herrera's liliipa uongozi zaidi  United's . 

Lakini  Leicester's walijikaza na kurejesha magoli hayo kupitia kwa David Nugent aliyefungwa kwa Penati na  Esteban Cambiasso na baadae jamie Vardy na penati ya a Ulloa ikawapatia ushindi Leceister city

18 September 2014

BALAA TUPU TIMU ZA UINGEREZA ZATEMBELEA SPANA MKONONI

  • Mchezaji wa Zamani wa man city na sasa   Bayern Munich's Jerome Boateng amefunga goli la ustadi wa Hali ya juu katika Dakika ya mwisho wa Mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya timu yake ya zamani ya   Manchester City na kuinyima walau alama moja .

    Mlinzi huyo wa zamani wa city Boateng alipiga kiki kali iliyoparazwa na kumshinda  Joe Hart baada ya city kushindwa kuokoa mpira wa kona .
    Hart aliokoa michomo kadhaa  kutoka kwa kina Thomas Muller, Mario Gotze na Boateng.
    City's walipata nafasi ya Dhahbu katika Dakika za mwisho wa mchezo pale Sergio Aguero alipomshinda  Dante lakini alipiga mpira uliotoka nje kidogo ya goli .

    Chelsea
    Kwa upande wa Chelsea Cesc Fabregas amefunga goli lake la kwanza katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya lakini halikuweza kumsaidia kocha  Jose Mourinho's kupata ushindi  baada ya Schalke kusawazisha goli hilo .
    Kiungo huyo wa Uispania , 27, aliyejiunga akitokea  Barcelona majira ya kiangazi alifunga goli hilo akipokea mpira kutoka kwa  Eden Hazard's .
    Didier Drogba alipiga shuti ambalo lilitoka nje ya goli na baadae  Klaas-Jan Huntelaar aliipatia goli la kusawazisha timu yake .
  • Bayern Mun 1 - 0 Man City FT
  • Roma 5 - 1 CSKA Moscow FT
  • Ajax 1 - 1 Paris St G FT
  • Barcelona 1 - 0 Apoel Nic FT
  • Chelsea 1 - 1 FC Schalke 04 FT
  • NK Maribor 1 - 1 Sporting FT
  • Ath Bilbao 0 - 0 Shakt Donsk FT
  • FC Porto 6 - 0 BATE Bor FT

17 September 2014

ARSENAL YACHARAZWA NA DORTMUND ,LIVERPOOL YASHINDA JIONI NI KLABU BINGWA ULAYA.

Szczesny collects the ball from the net

Klabu ya Arsenal's imeanza vibaya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya katika kundi  D mara baada yaa kutandikwa magoli mawili Dhidi ya miamba ya ujerumani Borussia Dortmund ambao walifunga goli kaika kila kipindi cha mchezo na kujihakikishia Ushindi .

Ciro Immobile alifungua sherehe ya magoli kwa Dortmund  Baada ya kumzidi Nguvu Laurent Koscielny na kumfunga  mlinda Mlango Wojciech Szczesny kwa shuti ya karibu.

Dortmund waliongeza goli la pili lilofungwa na Pierre-Emerick Aubameyang lakini kwa mara nyingine tena ,
Danny Welbeck alipoteza nafasi ya kufunga kwa arsenal  wakati mchezaji mwenzake  Aubameyang naye alingongesha mwamba . 
Mario Balotelli scores his first Liverpool goal
Steven Gerrard's alifunga pernati katika dakika za mwisho wa mchezo na na kuipatia Liverpool ushindi wasio utarajia wa magoli mawili kwa moja  2-1 tangu warejee katika ligi ya mabingwa barani ulaya.

Mario Balotelli alifunga goli la kwanza akiwa na jezi ya majogoo akigeuka kwa ufundi na kumfunga mlinda mlango wa Ludo Razgd na kupata goli la uongozi katika dakika ya  82nd-.
Lakini vijana kutoka katika jiji la Sofia nchini  Bulgarian waliasawazisha katika dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza pale mchezaji aliyeingia kutoka Benchi  Dani Abalo kuisawazishia timu yake . 

Gerrard, mchezaji Pekee aliyesaria katika kikosi kilichotwa ubingwa wa ulaya mwaka 2005 , ndiye aliyeisaidia timu baada ya   Javi Manquillo kufanyiwa  faulo na Mlinda mlango   Milan Borjan.
MATOKEA MENGINE 

14 September 2014

MAXIMO ANATUELEZA KUWA HATUNA MSHAMBULIAJI WA AINA HII


Wengi tulivyokuwa hatuna aibu hata ya kushngaa tutaanza kumsifia mchezaji mpya wa Daraja la Chini kule Brazil  Genilson Santana Santos ‘Jaja’ ambae leo amejichotea sita za bure mbele  ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Binafsi nimemtazama mara kadhaa katika mazoezi ya yanga paleLoyola la msingi ni kuwa Kocha Marcio maximo Tangu akiwa katika timu ya taifa ya Tanzania leo amewatukana Rasmi watanzania  tena kisomi  kwa kuwaeleza kuwa Hatuna mshambuliaji .

Binafsi ukimtazama Jaja ni mchezaji mbaye ana umbo kubwa mwenye mwili mzito kidogo lakini mwingi wa akili ukitazama goli la kwanza na la pili jaja amezoea kufunga tangu akiwa kwao Brazil .
Marcio alivyokuwa Timu ya taifa ya Tanzania alikuwa mara kadhaa akitafuta washambuliaji na wamepita wengi lakini leo ameaumua kuwaeleza ukweli kuwa hakukuawa na mshambuliaji katika timu ya taifa ya Tanzania
Binafsi nimeanza kuiona yanga ambao sikuwa kuiona kabisa kwa miaka mingi fizikia ,umakini wa viungo uimara wa safu ya ulinzi wakati fulani tuwe tunashawishika kuangaalia Sayansi ya soka inakwendaje lakini sio kupiga zogo tu ohooo yanga ,yanga simba ,simba, Azam kiboko yao swala kubwa wachezaji na uwelewa kwa walimu nadhani leo marcio maximo katufundisha jinsi ya kuwa na mshambuliaji anayejua kufunga . 

Si ajabu watu wataanza kukumbuka na kuanza kusema arejeshwe kwenye timu ya taifa ndio tulivyo sisi tuna ulimbukeni wa hali ya juu kweli ni kipi hasa tulichomwondolea Maximo leo anakuja kukifanya katika ardhi ya Tanzania tena kwenye timu yetu ya kizalendo sasa shida nini ? 
Hatuna wafungaji magoli tunawabahatisha magoli kwa miaka miwili iliyopita mfungaji bora katika nchi nyingine kwenye ligi yetu hii ni aibu tosha 
Leo kule kwenye magazeti ya Kireno Brazil watashangaa kuona kijana asiyejulikana katika fukwe za kopa capaba anaonekana Dhahabu hapa ndipo tunapoonyesha kiwango chetu cha juu cha ujinga tulinao ambao maximo katufundisha hakuna mafanikio ya Haraka katika soka .

MAN U ACHA SHETANI LAZINDUKA LAUA 4 SIFURI

Angel di Maria and Wayne Rooney

  • United imeshindaa mechi ya kwanza ikiwa na Van Gaal reign
  •   Mchezaji wa mkopo Falcao Aanzia kwenye Benchi 
  • Di Maria na  Herrera wamefunga magoli yao kwanza Leo
Manchester United imepata ushindi wa kwanza katika msimu huu na kuifunga timu ya QPR iliyoonekana kuwa dhaifu katika Dimba la Old Trafford. 


Mchezaji aliysajiriwa kwa Bei mbaya zaidi  Angel di Maria alioneka kuwa mchezaji bora zaidi katika mechi hiyo pale alipopiga mpira wa adhabu Ndogo na kwenda mbali kidogo kwenye kona .

Ander Herrera alifunga katika dakika ya 36 na baadae rooney akafunga kablaya kwenda mapumziko .


Juan Mata naye aliipatia United goli la Tatu kabla ya  akipokea pass kutoka kwa Di Maria's Radamel Falcao Aliingia kipindi cha katika dakika ya  67.
Mpaka mpira unakwisha Man u imeibamiza QPR goli nne bila na Di maria amekuwa Man of Match 

Mayweather WBA NA WBC MAIDANA HOI

.Floyd Mayweather versus Marcus Maidana

Floyd Mayweather AMSHINDA Marcos Maidana na kubakiza mikanda yake katika uzito wa  welterweight

Floyd Mayweather anaendelea kuwa Bingwa wa mikanda ya  WBA na WBC welterweight Baada ya kushinda kwa points Dhidi ya  Marcos Maidana huko  Las Vegas.
Ameendeleza ushindi wake wa mara ya tano bila kupoteza Mayweather's ajapigwa katika mapambano  47 .
Katika kucheza kwake ngumi ilikuchukua Sekunde kadhaa katika maisha ya miaka kumi nane na kucheza ngumi  kijana huyu mwenye miaka  37-alipata ushindi kutoka kwa majaji wote watatu
Katika Mzunguko wa nane, Mayweather alimshtaki  Maidana kwa kung'ata malalmiko ambayo Raia huyo wa Argentine aliyakataa .
Tukio hilo lilitokea pale walipokuwa wakipambana  katika kona ya ulingo .

Floyd Mayweather CV 

Alizaliwa: 24 February 1977, Grand Rapids, Michigan
Kama Bondia wa Ridhaa : Ameshinda 84 , Kapigwa mara sita . Ameshinda glove tatu za dhahabu . Medali za Shaba katika michuano ya 1996 ya Olympics
Akiwa Bondia wa Kulipwa : 11 October 1996
Professional record: 47 Kashinda  (26 KOs),Hajapigwa  .

"Tlukiwa tumekumbatiana na Sikuweza kugundua nini kilitokea ," anasema  Mayweather. "Baadae nikaona kaning'ata . Baaada ya mzunguko wa nane vidole vyangu viliumia , sikuweza kutumia mkono wangu wa kushoto .''
Majaji wawili waliamua mzunguko wa  12-kwa kunipa alama  116-111 na mzunguzko wa Tatu nikapata   115-112 na kuwa Bingwa na hii ilikuwa nzuri kwangu tangu nishinde kwa mfumo huo mwezi   May.
Floyd Mayweather
Mayweather alikiri kuwa Maidana alimuuma kwenye kiuno katika mzunguko wa nane

Mayweather ameripoitwa kutwaa kiasi cha Dolla $32m (£19.6m) katika pambanao hilo na katika masiha ya mchezo huio ameingiza kiasi cha  zaidi ya  $100m (£61.5m) katika miaka yake mitano iliyopita .
Maidana, 31, ambae anaoneka kama angerudiana kwa mara ya tatu na  Mayweather, alihitaji kuongeza juhudi zaidi kama angeihitaji ushindi 

Floyd Mayweather versus Marcus Maidana
NGUMIII KWENDA MBELE
Floyd Mayweather versus Marcus Maidana
POOOF 
Floyd Mayweather versus Marcus Maidana
NIMESHINDAAA !!!

13 September 2014

MADRID CHALI YALAMBWA 2 -1 BERNABU

Atletico Madrid
 
Atletico Madrid imepata ushindi na kulipiza kisasi cha kufungwa na Real Madrid  katika ligi ya Mabingwa ulaya baada ya kuwafunga katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu . 

Mabingwa watetezi wa La Liga  Atletico walipata Goli  la kuongoza katika Dimba la Bernabeu wakati  Tiago alipofunga kwa kichwa kwa mpira wa kona  . 

Cristiano Ronaldo,alifunga goli la kusawazisha akitokea kwenye majeruhi  kwa penati , na kuifanya Madrid kusawazisha  .
lakini Atletico, ambao walijitahidi kukabiliana na kelele za mshabiki wa Real , walishinda mechi hiyo kwa goli lililofungwa na  Arda Turan's .

WENGER AKIRI JERAHA LA Mathieu Debuchy NI KUBWA SANA

Beki wa kulia wa Klabu ya Arsenal Mathieu Debuchy ameumia vibaya na haijajulikana bado  atakaa nje ya kiwanja  kwa muda gani  .

Kocha  Arsene Wenger amesema majeraha ya  Debuchy’s  ‘Hayaonyeshi kupona upesi na kuna hitajika kufanyika uchunguzi wa kina zaidi waweze kugundua atakaa nje kwa muda gani .
Mchezaji hyuo mwenye 29- Debuchy alianguka vibaya na kukanyaga vibaya kifundo chake cha mguu wa kushoto  katika kipindi cha pili cha mchezo kati ya Arsenal na Mna city ambapo mchezo huo uliisha kwa magoli mawili kwa mawili katika mchezo uliochzwa jumamosi Tarehe kumi na tatu 

Arsenal defender Mathieu Debuchy screams in pain after injuring his ankle against Manchester City
Beki wa kulia wa Arsenal akigaragara chini mara baada ya kuumia kifundo cha mguu 

Gunners manager Arsene Wenger has admitted that Mathie Debuchy's injury 'doesn't look good'
Kocha wawashika Bunduki  Arsene Wenger Amekubari kuwa Majeraha ya  Debuchy's hayaonyeshi dalilia Nzuri

Mathieu Debuchy is taken off on a stretcher after suffering a badly sprained ankle at the Emirates

Arsenal Haina walinzi mbadala katika safu yake ya ulinzi ,Kijana mwenye miaka  19- Calum Chambers aliingia kuchukua nafasi ya mfaransa  huyo aliyetolewa kwa machera .

Debuchy alijiunga na  Arsenal katika majira ya kiangazi akichukua nafasi ya Bacary Sagna, ambaye amejiunga na klabu ya Man City, na alicheza vizuri katika mechi na klabu yake ya zamani katika uwanja Emirates.

Martin Demichelis ndiye aliyeokoa city kwa kusawazisha goli na kuipa alama moja  katika dimba la  Emirates .

Manchester City defender Martin Demichelis (right) celebrates after scoring a late equaliser against Arsenal

SIMBA 3 TIMU YA ZANZIBAR 3

 
Mchezaji wa zamani wa timu ya Annur na Malindi Ali Adof akipongezana na mchezaji wa zamani Simba Madaraka Suleiman. baada ya mchezo wao kumalizika kwa kutoka sare ya 3--3.
 
 
Wachezaji wa zamani wa Timu ya Simba wakiwa na wachezaji wa zamani wa Timu ya Taifa  na ya  Zanzibar wakipongezana baada ya mchezo wa kirafiki kumalizika kwa sare ya mabao 3--3, mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.mwenye jezi namba 18 Shem Frenk na jezi namba 15 Mbengu Mohammed.

KUMEKUCHA LIGI YA UINGEREZA MAKOCHA WAANZA KUKALIA VITI VYA MOTO

Pardew out banner 
Mshambuliaji  Graziano Pelle aliifungia mara mbili  Southampton na kuibamiza vibaya kikosi kilichocheza vibaya cha  Newcastle katika Dimba la Mtakatifu  Mary's .

Mtaliano huyo alifunga goli lake la kwanza katika dakika ya sita ya mchezo alipoungansha kwa Kichwa   Krosi ilitokea upande wa Kushoto ikipigwa na Ryan Bertrand's .
Alifunga bao lake la Nne katika msimu huu baada ya maamuzi mabaya ya Mike Williamson katika safu ya Ulinzi ya Newcastle .
Jack Cork alifanya kazi ya ziada baada ya uzembe uliofanywa na Williamson kabla ya Morgan Schneiderlin Kufunga Bao la nne 
Diego Costa 
Diego Costa amefunga magoli matatu katika mechi yake ya Kwanza wakitokea nyuma na kuibamiza Swansea na kuendeleza takwimu yao ya asilimia mia ya ushindi 100% tangu msimu wa ligi kuu uanze . 

Swansea ndio waliokuwa wakwanza kupata goli baada ya John Terry kujifunga akiokoa mpira wa Krosi lakini Costa alisawazisha kabla ya Nusu ya kwanza ya mchezo kumalizika .

Chelsea's iliendelea kuwa bora na   Costa alifunga akipokea pasi kutoka kwa  Cesc Fabregas .
Mshambuliaji huyo wa Uhispania alimtengea mpira  Ramires ambaye alipiga shuti lilompita  Lukasz Fabianski na  Loic Remy akafunga goli lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo lakini  Jonjo Shelvey's alifunga goli la kufutia machozi  .
Matokeo mengine katika ligi ya uingereza ni kama unavyoyaona hapo chini

ARSENAL VS MAN CITY PIGA NIKUPIGE 2-2

 

Goli la kusawazisha katika dakika za mwisho lilofungwa na  Martin Demichelis limeipatia  Manchester City point moja Dhidi ya Arsenal katika mechi iliyochezwa mapema mchana wa leo na iliyokuwa ya kuvutia .


Mabingwa watetezi walipata Goli la kuongoza kupitia kwa  Sergio Aguero's aliyefunga akipokea Krosi kutoka kwa  Jesus Navas's baada tu ya mchezaji mpya wa  Danny Welbeck kugongesha mlingoti katika siku yake ya kwanza ya mechi hii akiwa na jezi za Arsenal. 
Sergio Aguero

Washika Bunduki walipigana na baadae  Jack Wilshere's alifunga goli zuri zaidi akiuganisha Voli kutoka kwa Alexis Sanchez.

Lakini uzembe wa kutomkaba Demichelis aliunganisha mpira wa kona , na city mara mbili waligongesha mwamba kabla ya mpira kumalizika .

8 September 2014

MIMI NI MPENZI WA ARSENAL LAKINI NAFANYA KAZI CHELSEAA "FABREGAS"

Blue shirt, red heart? Cesc Fabregas has admitted that he will always love Arsenal 

Kiungo wa kati wa Uispania   Cesc Fabregas amesema amejikita kikazi katika klabu ya soka  ya Chelsea, lakini ataendelea kuwa mshabiki wa  moyo wake wote wa  Arsenal . 
Mchezaji wa huyo wa zamani wa washika Bunduki wa London na nahodha wa  zamani wa timu hiyo  anajiskia sawa kufanya kazi akiwa chini ya Kocha mreno  Jose Mourinho,huku  Arsenal ikiamua kutomnunua tena kiungo kutoka Barcelona kurudi kwenye Dimba la  Emirates . 
Fabregas, 27, alijiunga  Arsenal akitokea klabu iliyomlea tangu utotoni  na kuendelezwa kuwa moja kati ya Viungo bora zaidi Duniani  , Kabla hajarudi  Nou Camp mwezi  August 2011.
alishinda taji la Ligi kuu ya Uispania, Kombe la Mfalme  na Kombe la Dunia miaka mitatu iliyopita katika timu ya taifa ya Uispania  , Kabla hajaamua kurudi katika ligi kuu ya uingereza katika klabu ya  Chelsea. 
Katika mahojiano na  Gazeti la Uispania( El Pais),yaani Nchi hii   Fabregas alielezea hisia zake kwa  Arsenal na kuwa haitambadilishia hata kama atashinda kila kitu akiwa na vijana wapya kutoka katika jiji la London  Chelsea. 

"Unadhani sikufikiria jambo hilo [Kuchezea wapinzani wa  Arsenal's ambao ni  Chelsea]. mimi nitakuwa mpenzi wa Gunner katika maisha yangu yote na Najua nitarudi katika mitaa ya  Highbury [kwenye uwanja wa Emirates] na  [itakuwa ] wakati maalum ,lakini kwa sasa nipo kikazi zaidi  ," Fabregas .
"Na kukumbusha kuwa Nilicheza fainali ya klabu bingwa ulaya na klabu yangu zamani nilipokuwa arsenal dhidi ya Barcelona [nikiwa na  Arsenal]na Niliaapa kuwa  ningefanya chochote kushinda mechi ile  – na nimekuwa mshabiki wa  Barcelona Tangu nilipokuwa Mtoto  . 

"Kwa hiyo nitakapocheza Dhidi   Arsenal Nitajua tu kuwa nipo kwenye Timu tofati y [Kwasasa ] Timu , ambayo nitanacheza ndio ndugu zangu na ndio ninao watetea . N anajua kuwa mashabiki wa Arsenal watanielewa,Na sina shaka na Hilo ."
."

7 September 2014

Prince Ali Bin Al-Hussein "FIFA IENDELEE KUTOA NAFASI ZA KUANDAA KOMBE LA DUNIA KAMA KAWAIDA "

Reason: FIFA vice-president Prince Ali Bin Al-Hussein insists it's vital that the World Cup has new hosts 

Makamu wa rais FIFA  Prince Ali Bin Al-Hussein ametoa fursa  ya kuendelea kwa shirikisho hilo Kuzizawadia Nchi nyingine nafasi ya Kuandaa michuano ya Kombe la Dunia  Nchi ambazo hazijawahi kundaa kombe Hilo japokuwa kulikuwa na Utata katika kuizawadia Qatar kuandaa michuano ya mwaka  2022 .

FIFA imeipa Fursa ya kuandaa michuano ya  2018na  2022 kwa Nchi za Urusi na    kama ilivyokuwa kwa  2010 kwa afrika kusini ,lakini kulikuwa na Taarifa zilizosema kulikuwa na vitendo vya Rushwa vilivyomhusisha Mohamed Bin Hammam katika gazeti  Sunday Times ambazo zilimuangusha makamu huyo wa rais wa zamani wa fifa ambapo iliripotiwa  kuwa alitoa rushwa kununua Baadhi ya Wapiga Kura kuipa nafasi  Qatar.

Kwa mujibu wa Mchunguzi wa Kanuni za uchunguzi za FIFA  Michael Garcia aliwasilisha ripoti yake mwezi May na ,huku zikihusisha kuwa mashindano ya kombe la Duania hayatafanyika sehemu nyingine yoyote ile Zaidi ya Qatar  2022 , Prince Ali amesisistiza kuwa ni jambo la kawaida kwa nchi zinazotaka kuandaa kombe hilo kupata uzoefu ktoka kwa Qatar .
Project: Qatar plan to accomodate all the visitors for the World Cup with state of the art facilities Wakati hivi viwanja vianaanza kuchorwa ilikuonesha jinsi vitakavyohudumu 
'Sikuwepo wakati wakipeleka maombi ya kuandaa mashindano hayo sasa siwezi kutoa maoni kuhusu  yaliyotokea  (kwa mwaka  2022). Nadhani kitu cha muhimu ni kuwa tutakuwa tuna makombe mawili ya Dunia tena mazuri zaidi.

'Ni jambo la muhimu kwa kombe hili likaandaliwa kila bara ili litembee Duniani kote ,mimi ni msimamo wangu  kuwa litawezekana  , Sasa inabidi tuwe na matumaini kuwa linaweza kufanyika kwa njia sahihi na kila kitu kinaweza kufanyika kwa ufanisi zaidi ili tufike mafanikio  ,bila kujari yatakuja maamuzi gani  .'

Prince Ali,ambaye pia ni Rais wa Chama cha soka cha  Jordan , alikuwa akizungumzia ujio wa kombe la dunia katika bara lake miaka nane ijayo '  -
Anasema : 'Ni jambo zuri kwa kila mmoja pale kombe la dunia linapoandaliwa katika bara lake . Nikisema hivo , Tunayofuraha kubwa sana kuandaa michuano ya kombe la dunia kwa Umri chini ya 17 kwa wanawake na kombe la dunia la mwaka  2016,Kwani nina furaha sana na kila kitu kitakuwa sawa .

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers